URU KUSINI WAPATA KITUO CHA AFYA

 URU KUSINI WAPATA KITUO CHA AFYA

Na Gift Mongi,Moshi



Ni dhahiri kwa sasa wakazi wa kata ya Uru Kusini katika jimbo la Moshi Vijijini wanapata ahueni ya matibabu baada ya kituo cha afya katika kata hiyo kukamilika.


Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hiki muhimu maana yake ni kuwa wale wananchi waliokiwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika maeneo jirani sasa adha hiyo yafika mwisho.



Grace Ullomi mkazi wa Uru Kusini anasema kukamilika kwa kituo hicho cha afya ni dhahiri kuwa serikali ya awamu ya sita inakusudia kutekeleza adhma yake yakusoheza matibabu kwa wananchi.


'Kweli tukubali haya ndio matunda ya serikali yetu pendwa katika kutuletea huduma za afya katika ngazi za chini jambo ambalo lilishindikana kwa kipindi kirefu'anasema 




Kwa mujibu wa Grace ni kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya ni jitihada za.mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi na diwani wa kata ya Uru Kusini Willhad Kitally ambao Kwa pamoja walionekana kujituma.


'Tuna mbunge mpambanaji lakini na diwani vile vile tuliwapa kipaumbele chetu na wakatusikia na ndio maana unaona mafanikio haya kwa sasa'anasema



Neema Mallya mkazi wa Uru anasema sifa pekee ziwafikie viongozi wao akiwemo mbunge Prof Patrick Ndakidemi na diwani Willhad Kitally kwa mpango wao walioufanikisha


'Serikali ya awamu ya sita ina mipango mingi ila kutokana na umuhimu wa hawa viongozi wetu yaani diwani na mbunge tumepata kituo hiki jambo lililosubiriwa kwa kipindi kirefu'anasema 


 Anasema  anaishukuru serikali kwa mradi huo wenye manufaa kwa wananchi wa kata ya Uru kusini, pamoja na kata za jirani, kwani umewapunguzia adha kubwa wagonjwa waliokuwa wanakwenda mbali kupata huduma za kitabibu na kitaalamu.


Mradi huu ni moja ya miradi ya kielelezo katika Kata ya Uru Kusini na Jimbo la Moshi Vijijini kwa Ujumla



0 Comments:

Post a Comment