Rais Samia Aongoza Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa

Rais Samia  Aongoza Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa




Leo, Februari 17, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa, yaliyofanyika nyumbani kwake Monduli Arusha. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wanasiasa kutoka vyama vya upinzani.



Wakati akitoa salamu za pole kwa familia na wananchi, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kufanya siasa za maridhiano na za kujenga hoja, kuheshimiana, na kustahamiliana bila kutikisa misingi ya utaifa. Amesema kuwa hii ni njia nzuri ya kumuenzi hayati Lowassa na vitendo vyake.


“Hapa tunapata somo kubwa sana la siasa za kujenga hoja, kuheshimiana, kustahamiliana na siasa za kuleta maendeleo huo ni ukomavu mkubwa wa kisiasa na ni njia nzuri ya kuchukua kama tunataka kumuenzi Lowassa na vitendo vyake,” amesema Rais Samia 



Amesema kuwa Lowassa ni kiongozi alieacha funzo kuwa watu wanaweza kutofautiana katika mitazamo na sera bila kuvunja misingi ya Utaifa wao.


“alichotufundisha ni kwamba tunaweza tukatofautiana mitazamo, misimamo na sera bila kutukanana kulumbana wala kutikisa misingi ya Utaifa na mshikamano wetu na bado tukaelewana” ameongezea Rais Samia.



Lowassa alifariki Februari 2024 akiwa anapokea matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam, kutokana na matatizo ya kujikunja utumbo, tatizo la mapafu, na shinikizo la damu. Ameacha mjane, Regina Lowassa, watoto watano, na wajukuu kadhaa, na atakumbukwa na jamii yake ya kifugaji ya Maasai kama kiongozi wao laigwanan Mkuu . 






Lowassa alifariki Februari , 2024 wakati akiendelea na matibabu katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar Es Salaam, kutokana na tatizo la kujikunja utumbo, tatizo la mapafu na shinikizo la damu.


Ameacha mke mmoja Regina Lowassa na watoto wa watano na wajukuu kadhaa ambapo  Lowassa kumbukwa na jamii yake ya kifugaji ya maasai ambaye pia alikuwa kiongozi wao Laigwanan kwa mchango mkubwa wa maendeleo

0 Comments:

Post a Comment