Hotuba ya Mbowe ilivyogusa hisia za waombolezaji maziko ya Lowass

Hotuba ya Mbowe ilivyogusa hisia za waombolezaji maziko ya Lowassa 


Katika kipindi hiki cha huzuni na maombolezo baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ametoa salamu za heshima zilizoambatana na kumbukumbu ya mchango muhimu wa Lowasa katika historia ya siasa za Tanzania.

Ameyasema hayo leo Februari 17,2024 wakati akitoa salamu baada ya maziko ya Lowasa yaliyofanyika nyunbani kweke ijijini Ngarashi wilayani Monduli mkoani Arusha.


Mjane wa Marehemu Mama Regina Lowassa akisali mbele ya jeneza lenye mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake Monduli Mkoani Arusha. 17/2/2025. Picha ya Ikulu




Mbowe amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba historia ya Lowasa inaandikwa kwa usahihi, akikazia umuhimu wa kutoacha neno "CHADEMA" linapozungumziwa mchango wake. 



"Unawezaje kuandika historia ya Lowasa ukasahau utumishi wake wa miaka minne kama mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, mgombe wa urais wa mwaka 2015 ambaye alijenga demokrasia kwa viwango ambavyo haijawahi kufikiwa na mgombea yoyote wa upinzani katika taifa letu hili," amesema Mbowe huku waombolezaji wakipiga makofi kukubaliana naye na kuongeza.



"Wenzangu mtatambua Lowasa alianza safari ya matumaini ndani ya CCM baada ya hapo mimi siyazungumzi, na baadaye akahamia safari ya mabadiliko ndani ya CHADEMA. Huyu alileta kasi ya mabadiliko ya demokrasia ndani ya nchi yetu.

"Lowasa alilifanya bunge la Jamhuri ya Muungano wazungumzwa kwa sababu ni hatua ya ujenzi wa demokrasia katika katika taifa letu,".


Mbowe ameweka wazi mafanikio ya Lowasa, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wabunge na madiwani wa upinzani, na kufanikisha ushindi katika majimbo na majiji muhimu nchini. Amesema kuwa kwa kufanya hivyo, Lowasa alionyesha uwezo wake wa uongozi na karama ya kuhamasisha watu.

"Huyu kiongozi aliongoza uchaguzi na kuwezesha vyama vya upinzani kupata madiwani 2000 karibu nusu ya madiwani wa nchi,"amesema Mbowe huku waombelezaji wakiendelea kupiga makofi na kuongeza


"Vyama vingine tofauti na CCM vikaongoza jiji la Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Moshi, Mtwara, Iringa na Mbeya. Hampaswi kupuuza historia hii viongozi wangu. Tunatakiwa wakati wote tumuenzi Lowasa kwa sababu ni katika ujenzi wa demokrasia na ujenzi wa taifa letu zote. 

"Lowasa ni muathirika wa mifuno yetu ya uchaguzi lakini alikuwa mgombea wa upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita. Halikuwa jambo dogo, ni kwa sababu ya karama yake".

Mbowe amekiri na kutambua kwamba Lowasa alikuwa sehemu muhimu ya safari ya demokrasia na mabadiliko ndani ya vyama vya upinzani, na hivyo kufanya uwezekano wa kuiua historia hiyo kuwa jambo lisilowezekana.

Aidha, Mbowe amempongeza Lowasa kwa ukweli na uwazi wake, akisema kwamba yeye ni mtu wa kujitolea na kufanya mambo makubwa katika serikali, CCM, na pia katika CHADEMA.

Ameelezea mchango wa Lowasa katika kujenga demokrasia na mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania, akibainisha kwamba alikuwa na kasi ya kipekee katika kuleta mabadiliko hayo.



Mbowe amewataka Watanzania kuenzi na kuthamini mchango wa Lowasa katika ujenzi wa demokrasia na taifa  na kuwasihi viongozi wote kuheshimu na kuenzi historia ya kiongozi huyo katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya taifa lao.

0 Comments:

Post a Comment