DC Arusha Achukua Hatua Madhubuti Kudhibiti Bei ya Sukari: Wananchi Kufuata Bei Elekezi ya Sh. 3,000 kwa Kilo

 

DC Arusha Achukua Hatua Madhubuti Kudhibiti Bei ya Sukari: 

Wananchi  Kufuata Bei Elekezi ya Sh. 3,000 kwa Kilo



Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fecian Mtahengerwa, amekuja na mpango wa kudhibiti walanguzi wa sukari jijini Arusha ili kuhakikisha sukari inapatikana kwa wananchi kwa bei ya shilingi 3,000 kwa kilo. Amesisisitiza kuwa jiji hilo halina changamoto ya upatikanaji wa sukari.



Tahengerwa, akishirikiana na wakala wa sukari wa TPC, Karim Dakik, wametangaza kupokea tani 70 ya sukari na kuwataka wafanyabiashara kuuza kwa bei elekezi. Wameonya dhidi ya watu kutoka mikoa mingine kununua sukari kwa lengo la kuiuza kwa bei ya juu, na kuahidi kusimamia uuzaji na kuwakamata wanaofanya hivyo.



Mkurugenzi wa Alpha Group Limited, Karim Dakik, amethibitisha upatikanaji wa sukari ya kutosha kwa wananchi wa Arusha. Ameonya wafanyabiashara wasiuze sukari kwa bei ya juu na kuelezea kuweka dirisha maalum kwa wananchi wanaohitaji sukari kiasi kidogo kwa matumizi ya nyumbani.


Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameahidi kukabiliana na tatizo la sukari ifikapo Februari 15 na kuwataka wananchi kuondoa hofu. Kilo moja ya sukari inauzwa kati ya Sh. 4,000 hadi 6,000, na Bashe amewaasa wafanyabiashara kufuata bei elekezi, akisema watakaokamatwa kuficha sukari watafikishwa mahakamani.



0 Comments:

Post a Comment