MWENYEKITI WA CCM ARUSHA AFARIKI


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Zelote Stephen, amefariki dunia jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.


Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mussa Matoroka, amethibitisha kupokea taarifa za kifo hicho leo jioni, Alhamis, Oktoba 26, 2023.

Matoroka alisema, "Ni kweli Mwenyekiti amefariki jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amekwenda kupatiwa matibabu... huu ni msiba mkubwa kwetu CCM, familia, ndugu, na jamii."

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuomboleza kifo cha Marehemu Stephen na kuandika maneno ya kusikitisha.

“Taarifa za kuondokewa na Zelote Stephen, Mwenyekiti wetu wa CCM Mkoa wa Arusha ni taarifa za kusikitisha sana. Kwani kwa hakika kifo chake kimetunyima fursa muhimu ya kuendelea kujifunza mengi na kuuishi uongozi wake.

“Mungu ameendelea kutufunza. Mipango yetu imekwama. Nenda Laigwanan. Nenda mzee wangu. Nilipokutembelea siku chache zilizopita hospitalini, ulinipa matumaini. Kumbe mipango ya Mungu ikabaki. Wewe ni shujaa, Nenda Kamanda."

0 Comments:

Post a Comment