Majaliwa Awataka Madereva wa Serikali Kuzingatia Sheria




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka madereva wa Serikali kuzingatia sheria zote za usalama barabarani. 

Alisisitiza kwamba kuwa dereva wa Serikali haimaanishi kuwa wako juu ya sheria za barabarani, badala yake wanapaswa kuwa mfano wa kuzizingatia kwa umakini.


Majaliwa alisema, "Ukiwa dereva wa Serikali haimaanishi kuwa uko juu ya sheria, bali kila dereva anapaswa kuwa mfano wa kuzingatia sheria zote. Madereva wa vyombo vya Serikali wanapaswa kutumika kama mfano kwa madereva wengine."


Waziri Mkuu aliongeza kwamba madereva wa Serikali wanapaswa kufuata maadili ya taaluma ya udereva wa Serikali, ambayo inawataka kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani. Alisema, "Madereva wa Serikali wanapaswa kuwa kioo cha jamii."



Akihutubia katika Kongamano la Chama cha Madereva wa Serikali, lililofanyika Morogoro, leo Oktoba 24, 2023 ,Majaliwa alisisitiza kwamba madereva hao wanaweza kuendesha magari ya Serikali bila kusababisha ajali iwapo watatii sheria zilizopo. 


Kongamano hilo lilikuwa na kauli mbiu "Dereva wa Serikali Bila Ajali Inawezekana: Kazi Iendelee."


Majaliwa alipongeza kauli mbiu hiyo kama utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020/2025 na kuelekeza Serikali kudhibiti ajali za barabarani kama ilivyoelekezwa.


Aidha, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali inaendelea kushughulikia changamoto za watumishi wa kada ya udereva na kuahidi kuendelea kuyashughulikia maombi na ushauri utakaotolewa na Chama cha Madereva wa Serikali.


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, alihakikisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na madereva hao kupitia Chama chao katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuongeza ufanisi wa kazi za Serikali.


Kuhusu stahiki za madereva, Waziri Bashungwa alisema kuwa suala hilo linaipa kipaumbele na kuwa waajiri wote watahakikisha kwamba madereva wote wamepewa barua za kuthibitishwa, hasa wale ambao hawajapata barua hizo kulingana na maelekezo ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa UmmaWadau wa kada ya udereva wa Serikali wanajadili jinsi ya kuzingatia sheria za usalama barabarani kama sehemu ya juhudi za kuongeza usalama barabarani nchini Tanzania

0 Comments:

Post a Comment