KAMISHNA ACHPR AOMBWA AKAJADILI NA RAIS SAMIA SUALA LA NGORONGORO LOLIONDO N MSOMERA


 

BAADA ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, (ACHPR) kusema ripoti yao kuhusu malalamiko ya wananchi wa Ngorongoro, Loliondo na Msomera itakamilika Februari  mwakani, wananchi na asasi za kiraia wameiomba tume hiyo ikutane na Rais Samia Suluhu Hassan kwa dharura kwani wanateseka.


Aidha, walimweleza Kamishna wa Tume hiyo ambaye anashughulikia Jamii za pembezoni Dkt. Litha Ogana ambaye aliongoza tume hiyo mwezi januari mwaka huu kija nchini kuwasikiliza wananchi hao, ajitahidi kufanya taratibu za kukutana na Rais Samia hivyo kabla ya kumalizika kwa vikao vyao mwanzoni mwa mwezi ujao.


Waliyasema hayo  Oktoba 24, 2023 wakati wa majadiliano kwenye kikao kilichoandaliwa na Taasisi za kimataifa za Amnesty international, Protection international Afrika, Minority Rights group international na Human Rights Watch ikiwa na sehemu ya Vikao vya pembeni vinavyoendana na kikao cha 77 Cha ACHPR kinachoendelea hapa jijini Arusha.

Akichangia mada kwenye kikao hicho, mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la CILAO, Odero Charles Odero alishauri taasisi hiyo inayosimamia  haki za binadamu na watu  Afrika kusaidia wananchi wa maeneo hayo kupata haki zao za kuishi kwenye maeneo yao bila kubughudhiwa na uhuru wa kujipatia vipato kihalali na kutoa maoni kama ilivyo kwa Watanzania wengine.

"Unasema wataandaa ripoti na wanasema inaweza kufika februari mwakani na huku watu wanaumia? kama wako 'serious' waitishe kikao cha dharura na serikali ili kupatia ufumbuzi changamoto  haya," amesema Odero na kuongeza

"Mama (dkt Ogana)  unajisikiaje kama wanawake wenzako wamekosa huduma ya afya ya uzazi kama watoto wadogo wanakosa chanjo hili pia lisubiri ripoti kweli?.

"Bahati nzuri tume ya binadamu mko hapa Arusha mnaonaje kabla ya tarehe 10 (Novemba 2023) au ukimaliza  hiki kikao muombe 'apointment'  na Rais wa Tanzania  mkazungumzie haya,". 


Maombi hayo ya NGOs na wananchi wa maeneo hayo yalitokana na hoja zilizotolewa na Kamishna wa Tume hiyo ambaye anashughulikia Jamii za pembezoni Dkt. Ogana  aliyesema kuwa taarifa ya tume hiyo inaweza kutolewa februari mwakani kwani kuna hatua mbalimbali zinapitiwa kabla ya kutolewa rasmi.

Alisema kuwa tume hiyo ilipotembelea Tanzania mwezi januari mwaka huu ilibaini mambo manne yanayolalamikiwa na wananchi wa tarafa za Ngorongoro na Loliondo mkoani Arusha na Msomera mkoani Tanga.


Dkt Ogana aliyataja mambo ya awali ambayo tume hiyo ilibaini ni  matumizi ya nguvu wakati watu wakuiamishwa Loliondo kutoka eneo la kilometa za mraba 1,500 na ukosefu wa kushauriana.


"Ngorongoro tulikutana na watu wanataka kuhama ila hawana uhakika wa  serikali kuwalipa fidia kulingana na vitu wanavyomiliki na kuna wale hawataki kuhama na suala la ng'ombe zao kufa baada ya kuipatiwa chumvi yenye sumu na NCAA.

Hata hivyo Kamishna hiyo alifafanua kuwa ,"sisemi mambo ya ripoti nyie ni wananchi kazi yetu ni kuwapa taarifa,".

"Afrika kuna changamoto nyingi, nyie mnasema mnaondolewa sababu ya wanyamapori kuna wale wanafukuzwa kwasababu ya madini sisi tutajaribu tuwezavyo kuandaa ripoti bila kuficha chochote serikali ndiyo itafanya utekelezaji, ya mapendekezo ya tume".



Dkt. Ogana alishauri kuwa mgogoro wa tarafa ya Ngorongoro na Loliondo na ule wa Msomera hautamalizwa na taarifa ya tume bali kwa kukaa pamoja  jamii kupitia viongozi wao na serikali .



Awali wakizungumza katika kikao hicho, Wakili Joseph Ole Shangay, Wakili Edward Porokwa na Mtafiti wa Shirika la Amnesty international Roland Ebole walieleza changamoto kadhaa za Jamii za pembezoni na kukosekana Uhuru wa kujieleza.


Wakili Oleshangay alisema, wamefanya jitihada kadhaa kutatua migogoro ya Ngorongoro na Loliondo ikiwepo kufikisha Mahakamani mashauri kadhaa lakini bado suluhu haijapatikana.


Wakili Porokwa ambaye ni mkurugenzi wa Shirika la PINGOs Forums alisema hofu imetawala Ngorongoro na kusababisha Asasi za kiraia hata vyombo  vya habari vya ndani ya nchi kushindwa kufanya kazi.


"Hata kuzungumza hapa watu wanahofu hawajui hali itakuwaje wakitoka hapa hivyo Uhuru wa kujieleza umepungua sana kutokana na mgogoro huu," amesema Porokwa


Amesema kuwa watu wa Loliondo na Ngorongoro mbali na changamoto nyingine za wanazopitia lakini  hali ngumu zaidi  wanayopitia kwa miaka miwili iliyopita ni kuminywa kwa haki ya kueleza yale wanayopitia.

"Kukosekana kwa taarifa , vitisho, utashangaa taarifa za uongo zinazotolewa kwa umma na vyombo vya habari na hatujui ni kiasi gani cha fedha kinachotolewa na serikali kuwafanya waandishi watangaze masuala ya uongo kuhusu Ngorongoro na Loliondo.

"Hali hiyo ilianza wakati watu walipoanza kuhamishwa Ngorongoro  kuelekea mMomera ambapo 'media' zimetumika kufanya propaganda kuanzia june 10 2022," 

"Kabla ya hapo wanajamii walieleza mapendekezo yao namna wataendeleza maeneo yao. Ilipofika Juni 9,2023 waliwakamata viongozi wa wananchi wakati serikali ikiweka mpaka na wananchi wakapewa kesi ya mauaji wakakaa magereza miezi sita kisha wakaachiwa kwa madai kuwa hawana nia ya kuendelea na kesi yao,".

Porokwa alihoji kuwa unategemea wananchi wataongeaje kudai haki zao wakati kuna hofu ya kukamatwa na kufikishwa polisi au mahakamani 

"Tunamalalamiko kiuusu tume ya Afrika ya haki za binadamu na watu ambayo ilifika Tanzania lakini maeneo waliyopelekwa yalisababisha wananchi wengi washindwe kutoa maoni. 

"Tunauhakika kuna 'indiginas people' wanaishi Tanzania. Tunataka tume ichukue 'note' kuwa hawa watu walioongea hapa wanaweza kuface consequences.

"Ifike mahali tuondokane na ukoloni, wamasai ni watu sio wanyama kwa sababu wakati tukija hapa mimi nilivaa kawaida nimeruhusiwa kupita bila shida ila Joseph amevaa rubega akazuiwa akitakiwa ajieleze hii fikra  ya kikoloni inapaswa kuachwa,"..


Baadhi ya wananchi wa Ngorongoro, Loliondo, Msomera, Mara na Malinyi na wawakilishi wa Asasi za kiraia ndani na nje ya nchi wakizungumza katika kikao hicho, waliomba tume isaidie kumaliza mgogoro katika wilaya ya Ngorongoro, Msomera na maeneo mengine ya Jamii za pembezoni Afrika.


Akichangia mjadala huo, mwananchi kutoka Msomera, Frank alieleza kuwa hata wao waliathiriwa na zoezi la serikali kuhamishia wananchi wa Ngorongoro  kwenye maeneo yao bila kuwashirikisha.

"Wakati watu wakihamishiwa msomera hatukushirikishwa na hakukuwa na ardhi ambayo haina watu hivyo wakati tulipotaka kuhoji tukawa tumeshazingirwa hatiwezi kuongea," amesema Frank nankuongeza.

"Sisi ndiyo tulioumia zaidi kwa sababu tumenyanganywa ardhi na hatutambuliki tunawashukuru PINGOs ilituwezesha kukutana na makamishna wa tume ya haki za binadamu na watu ya Afrika tukawaeleza ilisaidia walau serikali walikuja kutusikiliza.

"Tunaomba tume itangaze ripoti yao,  sasa hivi tumeumia zaidi tumenyang'anywa ardhi wanawapa wenzetu tutakuwa na amani kweli?.


Naye mwananchi wa tarafa ya  Ngorongoro, Neema amesema kuwa baada ya serikali kuzuia miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao hali ya huduma muhimu za afya zimekuwa zikipatikana kwa shida hali inahowalazimu kuzifuata kwenye wilaya ya Karatu.


Amesema kuwa kwenye tarafa hiyo wanategemea mifugo kwa ajili ya kujipatia kipato ambapo kwa sasa hali ni mbaya baada ya mifugo hiyo kufa mwaka 2022 baada ya kula madini ya chumvi yenye sumu.




"Kwa sasa wanawake wengi wako Karatu wanatafuta fedha kwa ajili ya watoto na wengine wanajikuta wakijiuhusisha na biashata ya ngono kwa ajili ya kupata fedha za kihudumia watoto wao," amesema Neema kwa masikitiko..



Awali Dkt Ogana ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazungumzaji kwenye mjadala huo alifafanua hatua zilizocjukuliwa na tume hiyo ya Afrika ya binadamu na Watu.

"Tulipokuja mwezi wa pili kazi yetu ilikuwa mbili ilikuwa tukutane na watu wa Ngorongoro lakini ilibidi twende na Msomera tukawasikilize wananchi  na twende Dodoma tukutane na viongozi wa serikali tuwaeleze ile kazi tuliyofanya na maoni tuliyopata,".

Alisema kuwa walienda tarafa ya Ngorongoro na walitembelea shule zinazolalamikiwa kuwa zimeharibika zinahitaji ukarabati na walifanya mikutano mpaka usiku ambapo baada ya haponwalienda tatafa ya Ngorongoro.

"Tulisikiliza watu wa Ngorongoro, Loliondo na NCAA tukaenda Msomera tukakuta changamoto nyingine ila serikali ikajaribu kujitetea kwa maeneleo tukaona shule maji. 

"Tuliitisha serikali itupatie ushahidi wakatuma timu kutuletea maoni/ majibu.Kazi ikawa kuangalia maoni yote tuliyochukua kwa serikali, NCAA na kutoka kwa wananchi tutafanya uchmbuzi tuangalie pale tunaona ni wazi tunaweka kwa ripoti pale tunaona hatuelewi tunaomba ufafanuzi.

"Kazi ya kuandika ripoti ni ngumu, tunaomba mtupe nafasi tuandae ripoti. Kwa hiyo tunaandika ripoti tukimaliza tutawapelekea serikali wakisema hapana tutazungumza nao tukimaliza tutakuja kwa wananchi  kufafanua,"

"Hatua ya pili baada ya serikali kutupatia maoni yao hapo ndiyo ripoti itatolewa...Ripoti haitamaliza shida. Viongozi wanatakiwa waende na ripoti kwa serikali mkae chini mtengeneze kamati ya viongozi ili mtatue shida,

"Sisi kama kamati ya haki za binafamu na watu ni kushauri  serikali hatuwezi kufanya kazi ya serikali.



0 Comments:

Post a Comment