WAZIRI wa
viwanda na biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amekipongeza kiwanda cha mgodoro
cha TANFOAM kwa kutengeneza bidhaa bora
na nzuri zinazokidhi viwango hivyo kupendwa ndani na nje ya nchi.
Aidha amekipongeza kwa kuweza kuuza bidhaa zake kwenye nchi za Afrika Mashariki huku akiwataka kuendelea na juhudi hizohizo ili kuweza kuuza bidhaa zao kwenye nchi zote barani Afrika.
Dkt. Kijaji amesema hayo leo Agosti 1,
2023 wakati alipotembelea hicho kilichopo Jijini Arusha kujionea shughuli
za uzalishaji magodoro na kisikiliza changamoto zinazowakabili .
Amesema kuwa Serikali inahakikisha inaweka mazingira bora kwa
wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kutatua changamoto walizonazo ili
waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
“Natamani
kuona bidhaa hizi zinafika soko huru la biashara Afrika nchi zote 54 zilizobaki
ukiacha Tanzania kwani bidhaa inayozalishwa inakidhi viwango vya
kimataifa na hata kutoka nje ya Bara la Afrika kwani uwekezaji ni mkubwa
na teknolojia ni kubwa kutoka kiwanda Cha Tanform Arusha,” amesema Waziri
Kijaji.
Dkt KIjaji amesema kuwa wizara yake inatekeleza Mpango wa
Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambapo moja msingi yake ni kuondoa
majukumu yanayofanana kati ya Taasisi ili kurahisisha ufanyaji biashara
na uwekezaji nchini
Akiongea na uongozi wa kiwanda hicho, Dkt. Kijaji amezitaka Shirika la viwango nchini, (TBS),
Mamlaka ya Mapato nchini, (TRA) na Wakala wa Vipimo Nchini, (WMA) kuacha kufanya
majukumu yanayofanana na kuzitaka kushirikiana katika kuwahudumia
wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza biashara na uchumi wa Taifa
Amesema wizara
itaenda kukaa na taasis hizo ili kuelewa kazi zinazofanyika na mwisho wa siku
wawe na sera inayohitajika sokoni ili kuendelea kurahisisha mazingira ya
ufanyaji biashara wa wafanyabiashara.
Aidha,
Waziri Kijaji alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha pamoja na uongozi wa mkoa
kubadili utaratibu wa kuyalazimisha magari yanayobeba bidhaa kutoka viwandani
kwa ajili ya kuzipeleka kwenye maduka kupitia kwenye mizani.
“Changamoto
ya magari yanayobeba bidhaa kutoka kiwandani kwa ajili ya na kupelekea dukani kutakiwa kwenda kwenye
mizani ndipo wayapeleke dukani hiyo siyo
sahihi hivyo namuagiza mkurugenzi wa jiji na mkuu wa mkoa na timu yake kubadili
utaratibu… changamoto isionekane ni safari ndefu hata kama wanataka kukusanya
mapato,” ameagiza Waziri Kijaji.
Waziri
Kijaji amesema kuwa wao kama wizara wanasimamia sera wataenda kuchunguza kama
ni chanzo cha mapato ama ni kweli wanataka kulinda barabara kwani huwezi kutoa
gari nje ya mji na kuirudisha haipendezi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa TANFOAM, Meshack Jimmy
ameishukuru Serikali kwa jitahada mbalimbali inazozifanya katika kutatua
changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji ili kuwawekea mazingira bora ya
ufanyaji biashara na uwekezaji.
0 Comments:
Post a Comment