KIWANDA CHA KWANZA CHA SIMU JANJA NCHINI CHAFUNGULIWA ARUSHA

 

SERIKALI imeupongeza uongozi wa kiwanda cha Tanzatech Elecrtonics cha jijini Arusha kwa kuwa kampuni ya kwanza kuitikia wito wa Rais, Samia Suluhu Hassan wa kuanza kutengeneza simujanja (smartphones) hapa nchini.

Pia Kampuni hiyo inaunganisha vishikwambi (tablets), kumpyuta za mkononi, (laptops) smart projectors, wifi na mifi routers, mita za luku za umeme, prepaid mita za maji, vifaa vya kupima vya madaktari, (electronics stethoscopes na multi-parameter health monitors)



Pongezi hizo zimetolewa leo Agosti 1, 2023 na Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu KIjaji wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa kwenye ziara yake ya siku moja jijini Arusha.

 

Amewapongeza kwa hatua yao ya kuwa wepesi kiwanda hicho ambacho ni cha kwanza nchini na ni cha pili kwa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC) ambapo kiwanda kingine kama hicho kinapatikana nchini Uganda.

Waziri Kijaji, amewapongeza sana kwa kuanza kwa kuunganisha vifaa hivyo na baada ya kusikia wito wa Rais wa kuwakaribisha wawekezaji kwenye eneo la teknolojia ya na wao kuamua kuanza mara moja



“Tunatamani tutengeneze wenyewe lakini hata hii ya kuunganisha vifaa hivi ndani ya Taifa letu tunajisikia fahari. Tunawapongeza sana kwa kuwa wa kwanza hapa nchini kuanza utekelezaji huu,” amesema Waziri Kijaji na kuongeza

…Jukumu la wizara yetu ni kukuza mawazo yote yanayolenga kwenda mbele, sisi tunalea kila mmoja kwenye wizara afungue milango ya kuwasaidia wafanyabiashara kama hawa ili waweze kusonga mbele kwa kuzingatia sheria zetu zote,”

 

“Mmesajili kampuni BRELA lakini ni vema mkasajili bidhaa zenu ili msijemkafika sokoni mkakuta kuna mtu tayari anatumia jina hilo hivyo fanyeni kazi kwa karibu na TMDA (Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba) ili waweze kukulinda na kukulea ili muweze kufanya vizuri zaidi kwenye soko ndani na nje ya nchi,”.

 

Hata hivyo, Waziri Kijaji aliwashauri Tanzatech kuona namna ya kuzalisha vifaa hivyo hapahapa nchini huku akisisitiza kuwa kama vifaa vyote vinaagizwa nje ya nchi na kinachofanyika hapa nchini ni kuunganisha tu kuna kitu kinapungua.

“Vijana wetu ambao tayari Taifa limeshawekeza ndani ya vyuo vyetu, wewe mwenyewe umesoma vizuri hivyo tuangalie ni kitu gani kifanyike ili kila kitu kizalishwe na kuunganishwa hapa nchini,” alisisitiza Waziri Kijaji.

 

…Kuna fursa ya kupeleka bidhaa kama hizi soko la  AGOA lakini tunaambawa angalau asilimia 40 ya malighafi iwe ni ya hapa nchini hivyo tuangalie namna huko mbele kila kitu kitengezwe hapa nchini najua hii inawezekana mkishirikiana na watu wetu,”.




Awali Mkurugenzi Mtendaji wa TANZATECH, Gurveer Hans alimtembeza kiwandani hicho alichokianzisha kwa kushirikiana na raia wa China kutokana na uzoefu walio nao lwenye teknolojia.



 

Hans akaeleza kuwa  alisikia wito wa Rais Samia alioutoa Juni 9, 2023 wakati akifungua mkutano wa baraza la biashara la Taifa ambapo alitaka kuwepo na kiwanda cha kutengeneza simu janja hapa nchini.

 


“Nina furaha kukuarifu kwamba sisi Tanztech Electronics Limited tuko tayari kwa kazi hiyo. Kwa sasa kwa mwezi mmoja tuna uwezo wa kuunganisha simu janja 40,000, vishikwambi 30,000, laptops 15,000, na smart projectore 10,000,” amesema Hans.

Amesema kmuwa kwa kuzingatia mpango wa Taifa wa maendeleo unaoishia 2025 unaolenga kuongeza uwezo katika sayansi na teknolojia kwa kuzingatia maendeleo ya kielektroniki wako kutengeneza bidhaa hizo kwa bei rahisi na kuwaunganisha vijana katika kazi hiyo.

“Tanzatech iko tayari kushirikiana na serikali katika kutoa bidhaa hizi mashuleni, serikalini na kwa watu binafsi kwa bei inayofaa,” amesisitiza Hans .

 

Hata hivyo aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwapunguzia au kuwaondolea ushuru wa vifaa wanavyoingiza nchini kwa ajili ya kuunganisha ili kupata bidhaa hizo kwa bei nafuu kwani itasaidia kupunguza gharama za uzalishaji.

 

Hans anadai kuwa kwa sasa gharama ni kubwa kwani wanalazimika kjulipia kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 ushuru wa kuagiza asilimia 10 jambo aliloahidi kuuza bidhaa hizo kwa bei nafuu endapo serikali itapunguza au kuondoa ushuru na kodi hiyo.

 

wanalipia ushuru huo ukiondolewa au ambavyo tunaagiza kutoka nje ambazo tunaziunganisha hapa nchini

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


0 Comments:

Post a Comment