SEED.CO YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA, MONGELA ATIA NENO

 





SERIKALI imeipongeza kampuni ya kuzalisha mbegu za nafaka na mboga ya Seed.Co kwa kuamua kaufanya uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mbegu na ghala la kuhifadhia bidhaa hizo utakaogharimu karibu shilingi bilioni 5 kwenye eneo la Kisongo mkoani Arusha .

 

Aidha imewahakikishia kuwa nao bega kwa bega kuhakikisha kiwanda hicho kinakamilika kwa wakati huku ikiwataka Seed.Co kuwapa taarifa endapo watapata changamoto au vikwazo vyovyote vilivyo ndani ya uwezo wa serikali waweze kuwaondolea.

 

Pongezi hizo zimetolewa Agosti 18,2023 na mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela wakati akizindua ujenzi huo kwa kuchimba msingi na kupanda mti kwenye eneo la ujenzi lililopo kata ya Kisongo wilayani Arumeru mkoani Arusha kunapojengwa kiwanda hicho.

 


Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Seed.Co, Morgan Nzwere alisema kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa Tanzania wakiendesha  shughuli  zao  kwenye maeneo ya kukodi lakini kwa sasa mahitaji ya mbegu yamekuwa makubwa zaidi hivyo wameamua kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda hicho  cha kuchakata mbegu na ghala la kuzihifadhia ili kuongeza ufanisi mara mbili zaidi .


 Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mbegu nchini, (TASTA) Dk Bob Shuma alisema wamekuwa wakihimiza makampuni makubwa ya mbegu yazalishe mbegu hapa nchini.

"Uwepo wa kiwanda hiki utaongeza ajira si tu za kiwandani bali pia kwa wakulima wetu ambapo mbali ya kuzalisha mazao kwa ajili ya kuuzia walaji lakini sasa watazalisha mazao kwa ajili ya mbegu watakazoziuzia kiwanda cha Seed.Co," alisema Dk Shuma na kuongeza.

 

 


 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya kuendeleza kilimo ukanda wa Kusini mwa Tanzania,(SAGCOT), Geofrey Kirenga, alisema kuwa SeedCo ni mojawapo kati ya wabia wakubwa wanaofanya nao kazi ambapo wamekuwaja nchini kufanya uwekezaji kwa kuitikia wito wa serikali wa kuongeza uzalishaji wa mbegu za mazao nchini.

 

 

 

 

0 Comments:

Post a Comment