CHINA YAIPA EAC MAGARI NANE


SERIKALI ya watu wa China imetoa Msaada wa magari nane  yenye thamani ya dola 400,000 za Marekani  sawa na zaidi ya shilingi milioni 950 za Tanzania kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC) kwa lengo la kuboresha uwezo wa taasisi hiyo katika kupanga na kuratibu mikutano na matukio kwenye ukanda huo.

Msaada huo unaojumuisha mabasi matatu na magari madogo matano aina ya 'double cabin pick-ups' umekabidhiwa rasmi leo Jumanne Juni 27,2023 na Balozi wa China nchini Tanzania na EAC,  Chen Mingjian kwenye makao makuu ya EAC Jijini Arusha.



Akiongea mara baada ya kusaini hati za makabidhiano balozi, Mingjian amesema kuwa pia wametoa vipuri (assorted motor vehacle spare parts)  na wameleta wataalamu wa kutoa mafunzo ya matumizi ya magari hayo kwa madereva na mafundi wa EAC.

Amesema serikali ya watu wa China itaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na  EAC katika kujenga uwezo, biashara, maendeleo miundombinu kwa lengo la kusaidia kukuza Demokrasia uwajibikaji na utawala bora.


"Magari haya yalikuwa yatolewe mwaka 2021 lakini kutokana na janga la Uviko-19 ndio maana limefanyika mwaka huu, " amesema balozi, Mingjian na kuongeza

China inatambua mchango wa EAC katika kudumisha amani  na mshikamano , kuboresha miundombinu kwenye ukanda huu, na namna kwa pamoja walivyopambana na janga la UVIKO 19 na kukusa uchumi, mtangamano na kufufua uchumi wa nchi za ukanda huu,".


"Tumekuwa tunasaidia katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kukuza Amani Demokrasia Utawala Bora na uwajibikaji utakaosaidia jamii ya watu wa Afrika Mashariki kupata huduma bora,".

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu mkuu EAC na Mkurugenzi wa sekta ya maendeleo ya Jamii, Irene Isaka ameishukuru serikali serikali ya watu wa China kwa msaada huo unaony3sha ushirikiano mzuri uliopo baina ya taasisi hizo.


Amesema kuwa Serikali ya Watu wa China imekuwa ikisaidia EAC latika nyanja mbalimbali ambapo kwa mwaka 2022 ilitoa ferha kusaidia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na jumuiya hiyo na mkutano wa nne wa viongozi vijana wa EAC

0 Comments:

Post a Comment