TURKISH MAARIF YAPONGEZWA KUKUZA VIPAJI, YAWA KINARA KWENYE MOCK


HALMASHAURI ya wilaya ya Arusha, imeishukuru shule ya Turkish Maarif Arusha kwa kutoa ushirikiano kwenye shughuli za kijamii ikiwemo zoezi la upandaji miti kwa ajili ya kutunza mazingira.


Aidha ameipongeza shule hiyo kwa kuzingatia utoaji wa elimu kwa vitendo huku ikiendeleza vipaji vya wanafunzi wao kwa lengo la kuwawezesha kutimiza malengo yao kutokana na ubunifu binafsi nje ya yale wanayofundishwa darasani.





Hayo yamesemwa leo Mei 20,2023 na mkurugenzi wa halamshauri hiyo, Seleman Msumi wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita kwenye shule hiyo ya kimataifa iliyopo Ngaramtoni ambapo hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na  Afisa Elimu Sekondary wa halamashauri ya wilaya ya Arusha, Menard Lupenza.

Amesema  uongozi wa shule hiyo uliojipambanua kwa kutoa elimu kwa vitendo huku ukiibua, kukuza na kuendelea vipaji vya wanafunzi ambapo kwenye mahafali hayo wanafunzi walionyesha vipaji vya kwenye maeneo mbalimbali.


"Halmashauri ya wilaya ya Arusha tunaishukuru shule ya Turkish maarif kwa kuwa na ushirikiano mzuri na halmashauri yetu katika shughuli mbalimbali hivi karibuni wamwshiriki kwenye ziezi la kupanda miti. Kupitia mkuu wa shule,(sekondari)  Heri Salum tumekuwa tunashirikiana sana," amesisitiza Msumi na kuongeza



....Mimi kama kiongozi wenu wa elimu wa halamshuri ya wilaya Arusha, tunategemea wanafunzi wote 18 (wa Turkish Maarif)  kupata ufaulu wa division '1.3' (daraja la kwanza kwa alama 1.3).Hii inajidhihirisha kutokana na matokeo ya mitihani ya majaribio ya kikanda (Arusha na Manyara) wamekuwa wa tatu na mock wamekuwa wa kwanza kwenye shule zenye wanafunzi chini ya 40, vijana hawa walifanya vizuri," 

"Kama wilaya tunaitegemea shule hii ituweke kwenye ramani nzuri kitaaluma hata mkoa Arusha tulishajiwekea malengo kama jina letu lilivyo juu kwa kuanza na herufi A basi na kwenye matokeo ya wanafunzi wetu tunatarajia mkatuweke juu kitaifa,".

Afisa elimu Elimu Sekondari huyo aliwaasa wanafunzi kuwa wameeleza kuwa wamefundishwa kwa vifaa na teknolojia ya kisasa pamoja na kujifunza lugha nne kiswahili, kiingereza, kifaranza na kituruki pamoja nza tamaduni basi wakatumie lugha hizo kama fursa ya kujiendeleza.


"Arusha ni kutovu  cha utalii,  hivyo kujua lugha mbalimbali ni moja ya mambo yatakayokuwezesha kufanya biashara ya utalii kwa ufanisi zaidi kwani itakuwezesha kuwasiliana na watalii kutoka mataifa mbalimbali," amesema Lupenza.

Ameataka shule kuendeleza juhudi katika utoaji elimu na malezi mazuri kwa wanafunzi huku akisisitiza kuwa matokeo ya vijana wanaohitimu anaamini yatakuwa mazuri hivyo yatasababisha idadi ya watoto kuongezeka kwani matokeo hayo yataendelea kuwatangaza kitaifa.

Halmashauri ya wilaya ya Arusha ina jumla ya shule za sekondari 58 kati ya hizo 11 ndiyo zenye kidato cha tano na sita ambapo mpango wa serikali imelenga kuhakikisha wanafunzi wanapata ufauli wa daraja la kwanza  na la pili.




Mkurugenzi wa shule za Turkish Maarif Arusha, Halil Server amema kuwa watahakikisha wanendelea kutoa elimu ya ubora wa kimataifa kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuzalisha wahitimu walio bora zaidi. 

"Mmeweza kuwa wanafunzi wa shule hii baada ya kudahiliwa na kukifhi vigezo vya ubora kitaaluma hivyo ni mihimu sana kwetu na mmetudhihirishia ubora wenu kwenye matokeo ya mitihani ya kanda na mock naamini mtakuwa wa muhumu na msaada kwa maendeleo ya Taifa lenu," Server amewaeleza wahitimu hao.


Mkuu wa shule hiyo ya sekondari, Heri Salum amewaambia wazazi hao kuwa waliwafundisha ipasavyo vijana hao aliowaita darasa la dhahabu  hivyo ana uhakika wamefanya vizuri mtuhani wao wa mwisho hivyo wasubiri matokeo.



Mwakilishi wa wazazi, Raymond Degera ameshukuru uongozi wa shule na waalimu kwa malezi ya vijana wao kwa kipindi cha miaka miwili aliodai kuwa walitumia muda mwingi zaidi shuleni kuliko nyumbani.

Ameipongeza serikali ya Uturuki kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia katika malezi ya watoto wa Tanzania na kuamua kufanya uwekezaji kwenye sekta ya elimu huku akiomba ushirikiano kati ya serikali ya Uturuki na Tanzania uendelee kwa manufaa ya wananchi wa pande zote .


Kwa upande wake, Jonas Mzava akisoma risala kwa niaba ya wahitimu ameupongeza uongozi wa shule kwa kuwatengeneza mazuri ya kusoma masomo yao ya sayansi na biashara kwa kuhakikisha wanakuwa na madarasa yenye vifaa vya kufundishia vya teknolojia ya kisasa, maabara na makataba yenye vitabu vya kutosha.

"Elimu niliyoipata ni elimu kwa vitendo iliyonijengea hali ya kutaka kujaribu na kuzidi kujua na kwa kuwa walitujengea mandhari mazuri ya kusomea na tulikuwa tukipata msaada kwa waalimu kila tulipohitaji hivyo niko tayari kwenda kwenye jamii na kuwa suluhisho ya changamoto zinazoikabili jamii," amesema Mzava ambaye alikuwa kaka mkuu wa shule.

Amewashauri wahitimu wanaporudi nyumbani na kuingia mitaani wahakikishe wanasimama kwenye misimamo yao  yenye manufaa na wajiepushe kujiunga na makundi yasiyo mazuri 'wasidandie magari kwa mbele'. 

Mhitimu mwingine,  Lulu Ayoub ambaye alikuwa dada mkuu amewasihi wahitimu kuendelea kusimamia misimamo yao katika elimu na maisha ili waweze kutimiza malengo yao na waepuke kuiga maisha na mienendo isiyo mizuri kutoka kwenye makundi.
 

" Mimi nilikuwa nasoma EGM (biashara Jiografia na hesabu)  hii shule imetufundisha vitu vingi wasichana wanasema hesabu ni ngumu lakini kwenye hii shule hapana hesabu utaijua vizuri unajifunza kila kitu mwalimu anakufundisha mpaka unaelewa," amesema Lulu na kuongeza

Amesema kuwa tamaa ndiyo inachangia watu kudandia magari kwa kufanya vitu ambavyo siyo sahihi kwa kuiga maisha ya wengine hivyo akasisitiza wanafunzi kufuata misingi waliyowekewa na wazazi na walezi wao 

0 Comments:

Post a Comment