MPANGO wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ally Mwinyi wa kuimarisha sera ya uchumi wa buluu imeanza kuzaa matunda baada ya wawekezaji na wageni wengi kuongezeka kwenye visiwa hivyo hali inayoelezewa kuwanufaisha wafanyabiashara waliopo.
Akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mmiliki wa hoteli ya kimataifa za Madinat Al Bahr, Rastom Merani, alisema kuwa kuanzia mwezi julai mwaka huu hoteli yake imekuwa ikipokea wageni wengi wakiwemo wafanyabaishara wakubwa wanaofika visiwani hapo kwa ajili ya kuwekeza.
Alisema kuwa naamini ujio huo wa wageni ambao mbali ya watalii pia wapo wafanyabiashara wakubwa wanaokuja kuwekeza wakiitikia wito wa Rais wa Zanzibar Dk Mwinyi ambaye amekuwa akihamasisha wawekezaji kuja kuwekeza Zanzibar huku akiweka mazingira, sheria na sera nzuri za uwekezaji.
"Wanapokuja wawekezaji wakubwa wanahitaji hoteli kubwa kama hii (Madinat Al Bahr) kwa ajili ya kufikia wakati wakiendelea na mipango yao ya uwekezaji.
Sisi tunaweza kufanya harusi tano kwa wakati mmoja, tunaweza kufanya mikutano sita kwa wakati mmoja, hii hoteli unahitaji saa moja na dakika 30 uweza kuitembelea na kuona maeneo yote," alisema Merani
Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar ilizinduliwa rasmi Agosti 2019 na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein lakini walikuwa na changamoto ya soko kwa kipindi chote kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 ambao uliathiri dunia nzima.
"Tumejitahidi kutafuta soko na sasa tumeanza kupata soko kwani kipindi cha miaka miwili nyuma hali ilikuwa mbaya kutokana na ugonjwa wa UVIKO 19.Hoteli yetu ina hadhi ya nyota tano hivyo imekidhi vigezo vyote vya kimataifa," alisema Merani na kuongeza.
... Hapa tuna vyumba 120 kati ya hivyo vitano vina hadhi ya kutumiwa na marais. Sisi tunaweza kuwaweka hapa marais watano kwa wakati mmoja,".
"Pia tunachumba cha gharama kubwa ambacho kinaweza kutumiwa na sultani. Marais au mfalme wakija Zanzibar wanaweza kukitumia.Hii hoteli imelenga kusaidia kutoa huduma za kumbi za mikutano ya kimataifa na kitaifa, sherehe, vyumba vizuri kwa wageni wa viwango vyote,".
Merani alisema kuwa alifikia uamuzi wa kuwekeza Zanzibar baada ya kuombwa na Dk Shein wakati akiwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa hoteli yake ya New Dodoma iliyopo jijini Dodoma mwaka 2006.
"Mimi ndiyo mwenye New Dodoma hoteli wakati Dk Shein akiifungua rasmi mwaka 2006 aliniomba nikajenge hoteli Zanzibar, aliniambia itaweka kumbukumbu ya miaka 100," alisema Merani na kuongeza.
...Lakini akaniambia nijenge hoteli si kama nyingine, hii ni 'palace' (ikulu) ya Masheikh huu muundo wa Oman ndiyo maana unaona kuna miundo ya kiarabu pale ndani kila dizaini unayoiona ni yangu mwenyewe,".
"Nimeijenga hivi kwa sababu Waarabu wamekaa Zanzibar kwa miaka 200 na bado legacy yao ipo,".
Merani alisema kuwa Makamu wa Rais wa wakati huo Dk Shein al8msaidia akapata kiwanja hicho kwenye eneo la Nungwi ambapo ametumia miaka suta kujenga.
" Tumejenga hoteli hii kwa mahitaji ya serikali na kwa bahati nzuri kimataifa wametuweka kwenye viwango vya moja ya hoteli 10 nzuri zaidi duniani na kwa miaka miwili mfululizo tumetambuliwa kama hoteli bora zaidi kwa Zanzibar," alijivunia Merali wakati akielezea uwekezaji wake huo visiwani Zanzibar.
Akieleza sababu zilizompelekea kujenga hoteli hiyo Zanzibar, Merali ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam, alisema kuwa alifikia uamuzi wa baada ya kuombwa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Zanzibar Dk Shein wakati akizindua rasmi hoteli yake jijini Dodoma.
Hoteli hiyo iliyo ufukweni mwa bahari ya Hindi imeajiri watu 280.
Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi amekuwa akikutana na wawekwzaji wa ndani na nje ya visiwa hivyo na kuwaeleza dhamira yake ya kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi yanayojumuisha ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya bandari, barabara, uimarishaji wa sekta ya nishati, ujenzi wa hoteli za kitalii, huduma za afya na elimu.
Kupitia mpango huo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wa kuendeleza uchumi wa buluu kuna fursa nyingine kama uch8mbaji wa mafuta na gesi pamoja na uvuvi kwenyw bahari kuu.
0 Comments:
Post a Comment