AJALI YAUA NANE, WAMO MAMA NA WATOTO WANNE

 


WATU  nane wamefariki baada  ya magari mawili kugongana uso kwa uso ambapo  miongoni mwa waliofariki  watano ni wa familia ya wilayani 
 Biharamulo Mkoani Kagera.


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, (RPC), William Mwampaghale amesema kuwa ajali hiyo  imetokea katika maeneo ya Busiri kwenye  barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahura Wilaya ya Biharamulo mnamo tarehe 11 Julai 2022.


Ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili RAF 129W likiwa na Treila lenye namba RL 4367 aina ya Mercedes-Benz lililokuwa likiendeshwa na Vicent Gakuba Mnyarwanda, (52), gari hilo lilikuwa likitokea Rwanda na kuelekea Dar es saalam lililogongana uso kwa uso na gari namba T. 626 DRX aina ya Toyota Succeed lililokuwa likitokea Nyamalagala na kuelekea Benako lililokuwa likiendeshwa na Nyawenda Bihela, (35).

ACP Mwampaghale amesema kuwa  ajali hiyo imesababisha vifo vya watu nane ambao ni dereva na mmiliki wa gari ya Toyota Succeed pamoja na abiria wake saba waliokuwemo kwenye gari hilo, huku watano miongoni mwao wakiwa ni wa familia moja (Mama na watoto wanne).

Alisema kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba RAF 129W Mercedes Benz, kuhama upande wa kushoto wa barabara na kuendesha upande wa kulia uliopelekea kugongana na gari dogo ambalo abiria wake wote wamefariki kwenye tukio ajali hiyo.


RPC Mwampaghale amesema kuwa 
Dreva huyo alijaribu kutoroka mara baada ya ajali lakini jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata katika kizuizi cha Kahaza Rusumo akiwa ndani ya lori linaloelekea Rwanda, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


0 Comments:

Post a Comment