RAIS, Samia Suluhu Hassan amesema ataendeleza mema yote yaliyoachwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli ikiwemo nidhamu, uadilifu na kupiga vita ubadhilifu.
Rais Samia ameyasema hayo Machi 17, 2022 wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa kumbukizi ya kifo cha Hayati Magufuli, wilayani, Chato mkoani Geita .
“Hivi karibuni tutafungua daraja la Tanzanite lililoko jijini Dar es salaam hii ilikua ndoto ya Magufuli na nitaiendeleza kwa kuboresha huduma za maji, umeme na miundombinu, ”amesema Samia
Amemwelezea Hayati Magufuli kuwa Kiongozi aliyepinga rushwa na ubadhirifu, na kusisitiza uchapakazi na uzalendo kwa Taifa.
Rais Samia amewaahidi wananchi wa Chato kuwa Serikali itakamilisha na kushiriki kuifungua miradi yote ya maendeleo ambayo imeshakamilika ikiwemo stendi mpya ya Chato, uwanja wa ndege wa Chato uliofikia asilimia 95 pamoja na kivuko cha Chato.
0 Comments:
Post a Comment