NDAKIDEMI AWAHAKIKISHIA MABOGINI KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA

 Na Gift Mongi,Moshi




MBUNGE wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amewakikishia wananchi wa kata ya Mabogini kupata maji safi na salama baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha milioni 500 kwa ajili ya mradi wa maji.



Mradi huo wa maji ambao tayri umeanza utekelezaji wake utaweza kuwahudumia wananchi wa vijiji vya Mtakuja na Mserekia na kuwa bado serikali itaendelea kuwaletea maendeo katika kutatua kero mbalimbali za kijamii zinazowakabili.



Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo wa maji Prof Ndakidemi alisema katika kuonyesha kuwa serikali inawajali wananchi wa kata hiyo


miradi mbalimbali imeshatekelezwa katika kata ya Mabogini ikiwepo ya ujenzi wa Madarasa 15 ya UVIKO 19 katika sekondari za Mpirani (8) na Mabogini (7) ambazo zimegharimu shilingi milioni 300.



"Mradi mwingine mkubwa unaotekelezwa Mabogini ni ule wa ujenzi wa barabara ya Gate Fonga hadi Kahe kwa kiwango cha changarawe wenye thamani ya Sh 358 milioni" alisema 



Awali akitoa taarifa, mhandisi  Kija Limbe kutoka mamlaka ya maji safi na usafiri wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) alieleza kuwa mradi huo una thamani ya Tsh milioni 500 na unatekelezwa na MUWSA kwa fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Mkopo wa UVIKO 19.



"Kila kitu kinaenda sawa na mradi huu utaenda kukamilika kwa wakati na kama mnavyoona vitu vyote tayari vimeshafika hapa nankazi inaendelea tunamshukuru raid wetu Samoa Suluhu Hassan kutupatia fedha kwa ajili ya mradi huu " alisema



Akiongea na wananchi katika mkutano huo wa hadhara, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini  Ramadhan Mahanyu alimshukuru Prof Ndakidemi kwa jitihada za kuitetea kata ya Mabogini na kuleta miradi ya maendeleo. 



Aliwashauri wananchi waendelee kuiunga mkono serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani kazi zilizofanyika kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja zinaonekana na kuwa zinawagusa wananchi moja kwa moja. 



Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mabogini Athuman Kitia  kwa niaba ya wananchi waliishukuru Serikali na hususani Mama Samia, Mbunge, Diwani na watendaji mbalimbali wa serikali kwa miradi inayoelekezwa na kutekelezwa katika kata ya Mabogini.




0 Comments:

Post a Comment