MKURUGENZI wa mashitaka nchini, (DPP) i amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi, ugaidi iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Hati hiyo imewasilishwa leo Machi 4,2022 na wskili wa serikali mwandamizi, Robert Kidando mbele ya jaji, Joachim Tiganga wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi aliyekuwa anasikiliza shauri hilo linalofuatiliwa kwa karibu na wengi ndani na nje ya nchi.
Hatua ambayo imepelekea Mbowe na wenzake watatu kuachiliwa huru mara moja.Mahakama hiyo ilikuwa inamshikilia Mbowe na wenzake watatu kwa kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma mbalimbali zikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.
" Taarifa hii tunaiwasilisha kwa njia ya maandishi, kwa maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba kuondoa mashitaka yote dhidi ya washitakiwa wote sababu zote zipo katika Nole Prosequi {ikimaanisha musimshitaki} ambayo tumeiwasilisha" ameeleza wakili wa serikali Kidando.
ILIVYOKUWA MAHAKAMANI HAPO
Jaji anaingia Mahakamani Saa 4:52 asubuhi
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu
Wakili wa Serikali Robert Kidando;Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo pamoja na Pius Hilla, Abdallah Chavula, Jenitreza Kitali, Nassoro Katuga,Esther Martin, Ignasi Mwinuka Mawakili Wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige Wakili wa Serikali.
[04/03 11:39] +255 784 624 079: Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na Paul Kisabo,Sisty Aloyce, Gaston Garubindi, Iddi Msawanga, Evaresta Kisanga,Maria Mushi, Nashon Nkungu, John Malya, Jeremiah Mtobesya, Fredrick Kihwelo, Dickson Matata, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.
Jaji; Shauri lilikuwa lina kuja kwa Utetezi, Je Mnahabati zozote za Wateja wenu
Peter Kibatala; Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Shauri lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Utetezi
Kwa Upande wangu tulifanya Maandalizi Mazuri Mimi John Malya, Dickson Matata, Fredrick Kihwelo na wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea.Tuliagana nao wakiwa na bashasha kabisa, kwamba Leo tunaendelea na Utetezi. Lakini Leo asubuhi tumepata taarifa kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya kwa hiyo hatuwezi Kuendelea. Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu
Kibatala ; Kwa ajili ya Washitakiwa Kuendelea Kujitetea, Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji.
Jaji; Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi
Wakili Peter Kibatala ;Tarehe 07 March 2022
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Utetezi, na tumewasikia Wenzetu Maombi Waliyo Wasilisha. Sasa tusingependa Kujibu Hoja hiyo, Kwa sababu na sisi tuna maombi Mengine.
Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako
Kwa hiyo Kkjibu hoja hiyo haitokuwa na Maana sana.
Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili
Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai.
Mheshimiwa Jaji Taarifa Hii tunaiwasilisha kwa Njia ya Maandishi, Kwa Maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba Kuondoa Mashitaka Yote dhidi ya Washitakiwa Wote
Sababu zote zipo katika Noel Prosecui ambayo tumeiwasilisha
Wakili wa Serikali Robert Kidando anapeleka Nyaraka Mbele ya Karani wa Jaji, na Karani anampatia Jaji
Jeremiah Mtobesya Mheshimiwa Jaji tumesikia taarifa ya Notes hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Wa Mashitaka, na Kwa Bahati Mbaya hatuwezi Kusema lolote zaidi ya Kusema tunaichia Mahakama, Kwa sababu Kifungu Kinatoa Maelezo Yote Kwamba Baada ya Kusema hivyo tunaichia Mahakama dhidi ya Amri zake za Mwisho
Jaji; Je umezungumza kwa niaba ya Defense Wote..?
Jeremiah Mtobesya Mheshimiwa Jaji naomba kila Mmoja aseme
Fredrick Kihwelo kwa niaba ya Mshitakiwa wa tatu tumesikia taarifa iliyotolewa, tunaichia Mahakama iweze Kutoa Amri
John Malya Mheshimiwa Jaji notes iliyotolewa inatushika Mikono wote, pamoja na Kujiandaa kwa ajili ya Kujitetea, Mikono yetu imefungwa na hatuwezi Kusema lolote, Tulitaka sana warudishe gharama zetu na mengine lakini wacha tusubiri maamuzi ya Mahakama
Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Nasisi tunaichia Mahakama, Sheria inajielezea wazi
Mahakama ipo Kimya Kidogo na Jaji Bado anaandika
Nje ni Kelele za Shangwe na vifijo watu wanaimba, Imebidi Mahakama Kufunga Vioo Vya Madirisha ili Kuzuia Kelele Kuingia Mahakamani
Baada ya Mahakama kusikiliza hoja iliyoletwa na wakili mwandamizi wa Serikali kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka hana nia ya kuendelea na kesi hii, na upande wa pili wakaridhia, Mahakama inasema shauri hili lililokuwa linawakabili washitakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe linaondoshwa mahakamani na washitakiwa wanaachiwa huru bila masharti.
''Kwa sababu kuna vielelezo vililetwa Mahakamani, naandaa amri ya kuviachia, na hivyo naelekeza Mkuu wa Magereza kuwaachiwa mara moja leo na si vinginevyo'', alisema jaji.
Julai 21, 2021: Mbowe alikamatwa
Kiongozi huyu mkuu wa Chadema alitiwa mbaroni huko jijini Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 21 mwezi Julai, 2021. Chama chake cha Chadema, kiliwataka wafuasi wa chama hicho kuingia mtaani kumtafuta baada ya juhudi zake za kumtafuta kukwama na hawajui walipo, baada ya Mamlaka kutosema lolote kwa muda kuhusu kukamatwa kwa Mbowe. Baadae Polisi walikuja kuthibitisha kumkamatwa na kwamba amesafirshwa kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam na kuunganishwa kwenye kesi ya ugaidi.
Taarifa ya Msemaji wa Polisi, David Misime ilisema kuwa Mbowe hakukamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza bali alifahamu tuhuma zinazomkabili.
Julai 26, 2021: Alifikishwa mahakamani
Mbowe alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka mawili ikiwemo la ugaidi. Baada ya kusomewa maelezo Mbowe hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka, kesi ikahairishwa hadi Agosti 5, 2021 kusubiri nyaraka ili ihamishiwe Mahakama kuu.
Agosti 6, 2021 Alisomewa Mashitaka
Mbowe ambaye ni kiongozi wa zamani wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) na wenzake watatu walisomewa mashtaka sita yakiwemo ya kufadhili vitendo vya ugaidi na kukusanya pesa kwa kufanya vitendo hivyo.
Mashtaka mengine ni kukusanya fedha kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi, kukutwa na silaha aina ya bastola na kukutwa na sare za jeshi kinyume cha sheria. Kati ya mashtaka hayo sita, Mbowe anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi.
Agosti 9, 2021: Rais Samia azungumzia Kesi ya Mbowe
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan licha ya kusema hawezi kuzungumzia zaidi kesi ya Mbowe kwa kuwa iko Mahakamani, aliiambia BBC kuwa mashtaka dhidi ya kiongozi huyo wa Upinzani hayakuchochewa kwa sababu za kisiasa.
Pamoja na mengine kauli yake hiyo iliibua mjadala mzito kwa wafuatiliaji wa kesi hiyo na siasa za Tanzania kwa ujumla.
Septemba 03, 2021: Kuanza kusikilizwa kwa kesi
Kesi hii ilianza kusikilizwa kwenye Mahakama kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ikitokea Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ambayo haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kisheria.
Septemba 6, 2021: Jaji Luvanda ajitoa kusikiliza kesi
Jaji Elinaza Luvanda alijitoa kusikiliza kesi hiyo kufuatia maombi ya Mbowi, kwa niaba ya washitakiwa wenzake kudai kuwa hawana Imani na Jaji huyo kama atatenda haki. Nafasi yake akapangiwa Jaji Mustapha Siyani.
Oktoba 20, 2021 Jaji Siyani ajitoa kusikiliza kesi
Jaji Mustapha Siyani alikuwa jaji wa pili kujitoa kusikiliza kesi hiyo kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Jaji kiongozi. Jaji Joachim Tiganga akachukua nafasi yake
Februari 13, 2022: Ushahidi Kufungwa
Ushahidi umefungwa Wiki hii Februari 13, 2021 kwa mashahidi 13 wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi wao. Kinachosubiriwa sasa ni uamuzi wa Mahakama Kuu hiyo kuamua leo kama Mbowe na wenzie wana kesi ya kujibu ama la.
Februari 18, 2022 mahakama yawakuta na kesi ya kujibu ambapo ilipanga Machi 4, 2022 waanze kujitetea
0 Comments:
Post a Comment