HIVI HAPA VIKWAZO ALIVYOWEKEWA ABRAMOVICH


Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich 55, amewekewa vikwazo na serikali ya Uingereza kama sehemu ya majibu yake kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.


Yeye ni mmoja wa wafanyabiashara saba matajiri wanaodaiwa kuwa karibu na ikulu ya Urussi kuwekewa vikwazo vipya, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kwa mali yao na marufuku ya kusafiri.


Orodha hiyo pia inajumuisha mabilionea Igor Sechin na Oleg Deripaska, ambao wote wanaonekana kuwa washirika wa karibu wa rais wa Urussi, Vladimir Putin.


Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alisema hakuwezi kuwa na maeneo salama kwa wale ambao wameunga mkono uvamizi huo.


Vikwazo vya leo ni hatua ya hivi punde katika uungwaji mkono usioyumbayumba wa Uingereza kwa watu wa Ukraine. 

"Tutakuwa watu wasio na huruma katika kuwasaka wale wanaowezesha mauaji ya raia, uharibifu wa hospitali na uvamizi haramu wa washirika huru," amesema  Johnson.


Uingereza ilikuwa imekabiliwa na shinikizo la kumuwekea vikwazo Abramovich, ambaye alisema alikuwa amefanya uamuzi mgumu wa kuiuza Chelsea FC mapema mwezi huu.


Hata hivyo Abramovich, amekanusha madai ya  kuwa na uhusiano wa karibu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Uingereza inasema Abramovich, ambaye anakadiriwa kuwa na mali ya thamani ya £9.4bn, ni mmoja wa matajiri wachache kutoka miaka ya 1990 kudumisha ushawishi chini ya Putin.

0 Comments:

Post a Comment