Mwanaume, Madirisha Kanyalu (60) amejiua kwa kujitumbukiza kwenye kisima baada ya kumuua mtoto wake Meshack Madirisha (miezi 11) pamoja na mkewe, Evodia Nyerere (27) kwa kutumia kitu chenye makali akimtuhumu mkewe kuchepuka na wanaume wengine.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul tukio hilo limetokea Februari 2,2022 majira ya saa 12 asubuhi katika maeneo ya kitongoji cha Mwamadulu kijiji cha Bulambila kata ya Mwalukwa wilaya ya Shinyanga.
“Evodia Nyerere (27) na mtoto wake aitwaye Meshack Madirisha mwenye umri wa miezi 11 wakazi wa kitongoji cha cha Mwamadulu kijiji cha Bulambila kata ya Mwalukwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga waliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu ya shingoni na Madirisha Kanyalu (60) ambaye ni mme wa marehemu wakiwa ndani ya nyumba wanayoishi,” amesema Kaimu Kamanda huyo na kuongeza.
“Mtuhumiwa Madirisha Kanyalu alitoroka baada ya tukio na kwenda kujitumbukiza kwenye kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake aliyokuwa anaishi na kufariki dunia”,.
0 Comments:
Post a Comment