ZUHURA YUNUSI ACHUKUA NAFASI YA JAFFAR HANIU IKULU

 


Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa Shirika la UtangazajiUingereza(BBC), Zuhura Yunus kuwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais -Ikulu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari Mosi, 2022 imesema kuwa Zuhura anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa majukumu mengine ambapo uteuzi rasmi umeanza Januari 30, 2022.

Hivi karibuni, Zuhura ambaye amepata umaarufu kupitia kipindi cha Dira ya Dunia cha BBC alitangaza kuachana na shirika hilo na kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC Swahili  aliyojiunga nayo tokea mwaka wa 2008.

Taarifa ya Zuhura kuondoka BBC zilikuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC 

0 Comments:

Post a Comment