WAJUE WAWAKILISHI WA URUSI NA UKRAINE KWENYE MAZUNGUMZO YA AMANI

 


Mazungumzo yanaendelea kwenye mpaka wa Belarus kati ya maafisa wa Urusi na Ukraine.

Ni mara ya kwanza wanakutana tangu Urusi kuvamia, lakini matumaini ya kufanikiwa si makubwa.

Kabla ya mazungumzo hayo, Ukraine ilisema inataka kusitishwa kwa mapigano na Urusi kujiondoa, huku Kremlin ikisema haitatangaza msimamo wake.

Wapatanishi wa Urusi wamezungumza kuhusu makubaliano ambayo yana maslahi ya pande zote mbili.

Ujumbe wa Ukraine unajumuisha Waziri wa Ulinzi Oleksiy Reznikov na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mykola Tochytskyi.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Alexander Fomin na Balozi wa Urusi nchini Belarus Boris Gryzlov pia ni miongoni mwa waliopo.

0 Comments:

Post a Comment