UBELGIJI KUJENGA KIWANDA CHA KUTENGENEZA DAWA ZA WATOTO,COVID NCHINI


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya  mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo, Brussels nchini Ubelgiji leo tarehe 17 Februari, 2022.


Katika mazungumzo hayo, De Croo amekubali ombi la  Rais Samia la kuisaidia Tanzania kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa kwa ajili ya watoto pamoja na kuzalisha dawa ya Covid.


De Croo alipongeza mtazamo wa Mhe. Rais Samia kuhusu usalama  wa ukanda wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na rai yake kwa mataifa mbalimbali kuunga mkono msimamo wa EU wa kufanya Burundi kuondolewa vikwazo.

0 Comments:

Post a Comment