SAMIA ; SIPENDI KUTUKUZWA WALA KULINGANISHWA NA MUNGU




 RAIS Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.


Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 wakati akihutubia kwenye sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 ya Uaskofu wa Askofu Severine Niwemugizi inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.


Alikuwa akijibu moja ya ombi la  Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi ambaye wakati akihutubia alilotoa kwa  Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.


“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine," amesema Rais Samia na kuongeza.



... Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.


Awali Askofu  Niwemugizi alimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.


“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile  usikubali."amesema Askofu Niwemugizi na kuongeza


"Ninakumbuka sana Hayati Benjamini Mkapa najua huko mlikuwa mmezoea mtukufu rais, mtukufu rais alifika mahali akawa mkali kabisa mtukufu ni Mungu tu naomba hilo liwe neno kwako, " .


...Basi nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza,  ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu."



na mshikamo wa Watanzania ili hatimaye utumishi wako utukuke na kuacha alama itakayoonwa kwa vizazi vingi.

0 Comments:

Post a Comment