ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya
ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema alishindwa kuwasilisha mahakamani taarifa ya
kutokuwa eneo la tukio kwani hakujua ajitetee hakuwa eneo lipi kati ya
yaliyotajwa mahakamano.
Ameyasema hayo leo
Februari 7, 2022 mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda
anayesikiliza shauri hilo la uhujumu uchumi namna 27/2021 kwenye mahakama ya
hakimu mkazi Arusha wakati akiongozwa kutoa ushahidi (re examination) na
wakili wake, Moses Mahuna.
Sabaya amesema
kuwa wakati akihojiwa maswali ya dodoso na mawakili wa serikali alionyeshwa
hati ya mashitaka kisha akaulizwa ni kwa nini hakutoa taarifa kuwa atajitetea
kuwa hakuwa eneo la tukio na akajibu hakujua ajitetee hakuwa kwenye tukio eneo
gani .
"Wakati anauliza
swali alinionyesha hati na kwa mujibu wa hati nilishindwa kutoa taarifa kwa
sababu sikujua najitetea sipo wapi na wakati ushahidi unaendelea uliletwa
maeneo mengi ambayo hayapo kwenye hati ya mashitaka hadi maeneo ya Dar es
Salaam yalitajwa tukashindwa kuelewa tunajitetea hatukuwa wapi," ameeleza
Sabaya.
Katika hatua nyingine
shauri hilo limeahirishwa mpaka Februari 16, mwaka huu kwani mawakili wa
utetezi wana mashauri mengine kwenye mahakama ya rufani ikiwemo shauri lingine
la Sabaya linalotarajiwa kusikilizwa Februari 24,mwaka huu hivyo
wanaomba muda kwa ajili ya maandalizi.
Wakili Mahuna
aliwasilisha ombi la kuahirishwa kwa shauti hilo mara baada ya Sabaya kumaliza
kutoa ushahidi wake ambapo alisema wanaweza kuleta shahidi mwingine mmoja
lakini kwa muda uliobaki wanaona hatamaliza kutoa ushahidi wake.
"Sababu ya kuleta
ombi hili baadhi ya mawakili tuna kesi kwenye mahakaman ya rufaaa kesho
tarehe 8,15 na licha ya kesi hizi tuna kesi nyingine ya rufaa
inayomhusisha mshitakiwa wa kwanza (Sabaya) na wa tano Silvester Nyengu
ambao wapo katika kesi hii," alieleza Mahuna na kuongeza.
...Na mawakili ni hawa
hawa na kulingana na 'nature' ya kesi inahitaji maandalizi ya kina na kutokana
na kesi zingine na kesi hiyo ya jumatatu tulikuwa na ombi kwamba mahakama yako
ionelee vema kuahiriaha shauri hili kwa leo hadi tarehe 16 Februari ili
tuendelee na mashahidi wengine waliobaki,".
Kwa upande wa Jamhuri
wakili wa serikali Mwandamizi, Janet Sekule alisema hawana pingamizi na ombi
hilo la upande wa utetezi huku akionyedha mashaka yake kuwa hawajaleta hati za
wito wa mahakama kuthinitisha kuwa kweli wana kesi kwenye mahakama ya rufani
kama wanavyodai.
"Hatuna pingamizi
na ombi la utetezi ingawaje hawajaleta hati za wito kuthibitisha kama wana kesi
kama wanavyodai tuko tayari kuendelea kwa tarehe waliyoomba kwani sheria iko
wazi kuwa panapokuwa na mashauri kwenye mahakama za juu mahakama za chini
zinasubiri," alieleza Wakili Sekule
Hakimu Kisinda alisema
kuwa amekubaliana na ombi la kuahirisha shauri hilo mpaka februari 16, mwaka
huu.
Wakili wa utetezi Moses
Mahuna akimuongoza Sabaya kuboresha ushahidi wake (re examination)
Wakili:Bwana Lengai
wakati unahojiwa na mawakili wasomi wa jamhuri uliulizwa swali ukajibu hukuona CCTV footage ikichezwa hapa mahakamani ulikuwa na
maana gani?
Shahidi:Sikuona footage
hiyo ikichezwa mahakamani na ni kweli sikuona sababu alikuja shahidi wa saba ambaye ni mtaalam wa CRDB akaieleza
mahakama kile alichokitoa kwa shahidi namba nane siyo kile alichokikuta
mahakamani maana yake kilikuwa kimebadilishwa, kimeongezwa alisema hivyo.Alikuja
shahidi wa tisa meneja wa benki Mary Kimasa akasema tarehe 1.6.2021 aliangalia
hiyo CCTV kule benki kwa Mrombo na hakumuona mtu yoyote aliyepo hapa mahakamani
katika footage hiyo
Wakili:Uliulizwa swali
ukajibu video iliyopo hapa sicho kilichotokea kwa Mrombo ulikuwa na maana gani
kujibu hivyo?
Shahidi:Nilikuwa na
maana kwamba ile video halisi niliyoona na shahidi wa saba na tisa siyo halisi
iliyoletwa mahakamani hasa baada ya kuingizwa kwenye mfumo mwingine na
kubadilishwa uhalisia wake. Na shahidi namba saba alikiri kuna vitu vimeongezwa
siyo halisi.
Wakili:Wakati unadodoswa
na wakili Kwetukia ulijibu unaonekana simu ipo TANAPA, White Rose, Haile Selassie
ulipokuwa ukijibu ipo katika hayo maeneo ulikuwa ukimanaisha nini
Shahidi:Kielelezo cha
tatu nilikuwa nasisitiza ni mawasiliano ya simu ilipo na siyo mtu kama
ilivyoelezwa na mtaalamu shahidi wa sita wa jamhuri
Wakili:Ulilizwa swali
kwa kutumia kielelezo cha tatu ukaonyeshwa mida mingi anakwambia
mawasiliano yalifanyika Mbauda ukasema ni kweli kulingana na kielelezo ulikua
na maana gani kusema ni kweli?
Shahidi:mimi nilikuwa
nasoma kielelezo P3 ambacho kwanza ni kielelezo kinachotaka maelezo ya
kitaalamu,nilieleza mahakama hii simu hiyo 0758 707171 alikuwa anatumia mke
wangu Jesca Thomas ambaye alikuja hapa kama shahidi
Maswali simu ilikuwa Mbauda
alipaswa kuulizwa yeye aliyekuwa anatumia simu siku hiyo, hawakumuuliza
chochote maana walikubalaiana naye. Kuniuliza mimi walikuwa wananionea maana
shahidi alikuwepo hapa
Wakili:uliulizwa swali
ukajibu kwa muda huo uliotajwa simu haikutoka Arusha ulikuwa ukimaanisha nini?
Shahidi:Mhe Hakimu
nilijuwa najibu kwa mujibu wa kielelezo mimi sikuwa na simu hiyo kujua ilikuwa
wapi na inafanya nini mimi nilipewa tu nisome na nilisema aliyetoka Arusha kuja
Boma (ng’ombe) ni mke wangu siyo simu na mimi nilimfungulia mlango usiku mke
wangu
Wakili:Uliulizwa swali ukajibu
hujui kwani shahidi namba mbili wa utetezi alitumia dakika 25 kupita Mbauda
akielekea Kisongo
Shahidi:Hizo dakika 25
zipo kwenye kielelezo ambacho ni ripoti ya kitaalamu ambayo ripoti hiyo kwa mujibu
wa mtaalum alisema inaeza kusoma umbali wa kilomita tano.
Shahidi wa pili (wa
utetezi Jesca) angeulizwa angeweza kueleza yeye na siyo mimi
Wakili:Hapa mahakamani
ulionyeshwa kielelezo P3 ukasema kwenye hicho kielelezo kuna incoming sms toka
kwa namba ya Enock Mneki kwenye namba ya mtu anaitwa Lengai Sabaya ulikuwa
unamaanisha nini
Shahidi:Kwa mujibu wa
kielelezo P3 mawasiliano yalikuwa yanafanyika Kati ya hizo namba mbili ambapo
nilisoma kwenye kielelezo na maana yangu ni kwamba waliopaswa kukielezea ni
wale waliokuwa wanatumia simu na siyo mimi
Wakili:Uliulizwa swali
akauliza kuna kipindi namba zilizosajiliwa kwa majina ya Enock na Lengai
ole Sabaya inaonekaa inasoma mnara mmoja sasa Sombetini two simu hizo zilisoma
mnara wa Sombetini two na ulipoulizwa
inaonekana kuna 8 transaction ikiwemo sms incoming calls ulijibu ndio, ulikuwa ukimaanisha
nini?
Shahidi:Aliniuliza swali
akisoma kielelezo nilikua namaanisha ndo kiliandikwa kwenye kielelezo hicho
Wakili:Kuna swali
ulijibu shahidi mmoja hawezi kuthibisha kesi ulikuwa na maana gani?
Shahidi:Nilikuwa na
maana ya kwamba ni kwa mujibu wa sheria ushahidi wa shahidi mmoja lazima
uchukuliwe kwa tahadhari sana kwamba katika mazingira ya mkanganyiko wa
ushahidi wake mwenyewe hapaswi kuaminiwa na kuthibitisha shtaka la jinai kama
hili atahitaji shahidi mwingine wa kumuunga mkono
Wakili:Uliulizwa hapa
habari ya DAS kwamba ulikuwa naye siku nzima kwanini hukumleta kama shahidi
ukajibu RAS alishawakilishwa na shahidi namba moja wa jamhuri na ushahidi wake
umethibitisha hukutoka ofisini tarehe 22.1.2021 na ulikua unamaanisha nini?
Shahidi:Nilikuwa namaansiha
shahidi namba moja wa Jamhuri ameieleza mahakama kwamba hana taarifa yoyote
toka kwa DAS kwamba mimi ela gari wala dereva havikutima hai 22.1.2021 na
akasema nilikuwepo ofisini siku hiyo na ningetoka lazima angefahamu na yule
shahidi ni mkuu wake DAS sikua na uhitaji wa kumleta DAS kwani alishaeleza
shahidi huyo
Wakili:Uliulizwa swali
pia ukajibu hukutoa taarifa mahakamani kabla ya utetezi kuwa hukuwepo wilaya ya
Arusha ulikuwa una maana gani kumaanisha kutoka taarifa mahakamani
Shahidi:Wakati anauliza
swali alionyesha hati na kwa mujibu wa hati nilishindwa kutoa taarifa kwa
sababu sikujua najitetea sipo wapi na wakati ushahidi unaendelea uliletwa
maeneo mengi ambayo hayapo kwenye hati ya mashitaka hadi maeneo ya Dar es
Salaam yalitajwa atukashindwa kuelewa tunajitetwa hatukuwa wapi
Wakili:uliulizwa kuhusu
kupekuliwa usiku na mali kuchukuliwa bila nyaraka je ukaulizea kufanywa hivyo
kunafanya wewe kuwa hujatenda makosa ukajibu ndio ulimanaisha nini
Shahidi:Kama sheria
inataka mtu asipekuliwe usiku bila kibali cha hakimu mtu yoyote anayefanya
hivyo hana tofauti na jambazi na maana yake ni kwamba yeye ndiye anakuwa mtu
aliyethibitika kuvunja sheria mimi nabaki kuwa mtuhumiwa na nilimaanisha huwezi
kuvunja sheria kwa madai ya kutafuta haki
Wakili:Uliulizwa hapa swali
kwamba umeleta nyaraka yoyote kuonyesha TAKUKURU baada ya mke wako kupeleka mkataba na kadi ya
gari,ukajibu hao hawafuati sheria katika uchukuaji wa mali ulikuwa unamaanisha
nini?
Shahidi:Nilimaanisha kwamba
TAKUKURU wamechukua mali zangu na wanachukua mali za watu bila kufuata
utaratibu wa kisheria kama walivyochukua gari yangu na vitu vingine…
Uthibitisho kwamba
wanafanya hayo uko hapa mahakamani kwa kuwa wameleta gari ambayo walipaswa
kuichukua kwa mujibu wa sheria akiwa ana hati ya ukamataji na risiti lakini
hati hizo na risiti hawajaja nazo hapa mahakamani wasingeweza kumpa Jesca
risiti kwani huo ni utaratibu wao wa kuvunja sheria kama walivyofanya kwenye
gari

0 Comments:
Post a Comment