SABAYA : SIJUI KWA MROMBO ILIPO, ADAI SI MMILIKI WA LAINI YA SIMU ALIYOSAJILI KWA JINA LAKE

 

 


 

ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameieleza mahakama hajui eneo la Kwa Mrombo kama lipo jijini na wilayani Arusha.

 

Aidha, amesema kuwa laini ya simu yenye namba 0758707171 ameisajili kwa jina lake lakini yeye si mmiliki na inatumiwa na mke wake, Jesca Thomas kwenye shughuli zake.

 

Ameyasema hayo leo mbele ya hakimu Mkazi, Patricia Kisinda wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha kwa nyakati tofauti wakati akiulizwa maswali ya dodoso na mawakili wa serikali Neema Mbwana, Ofmed Mtenga, Felix Kwetukia na mwendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, (TAKUKURU), Richard Jacopia.

 


Sabaya alidai kuwa kuanzia siku ya kwanza amesomewa mashitaka mahakamni hakujua kama Kwa Mrombo iko jijini Arusha licha ya kuwa amewahi Mwenyekiti wa UV CCM mkoani Arusha .

 

Sehemu ya mahojiano ya wakili wa serikali mwandamizi, Kwetukia  na Sabaya . 

 

 

WAKILI:Wewe ni mzaliwa wa Arusha na ulishawahi kuwa Mwenyekiti  wa UVCCm mkoa wa Arusha 

SABAYA:Ndio

WAKILI:Unafahamu kuwa kwa Mrombo ipo jijini na wilaya ya Arusha

SABAYA:Sifahamu

 

Wakili Kwetuki akaomba hati ya mashitaka kwa hakimu na kumtaka Sabaya aisome mashitaka yote matano ambayo katika kusoma kwake alimuelekeza asome sehemu iliyoandikwa wilaya na maeneo mbalimbali katika wilaya ya Arusha.

 

WAKILI:Kuanzia siku ya kwanza ulielewa kuwa kwa Mrombo ni ndani ya wilaya na jiji la Arusha

SABAYA:Sikuelwa kwa kuwa hati ipo disputed

 

WAKILI: walikuja baadhi ya mashihidi hapa makahamani wakataja maeneo hapa Point zone, walieleza Mbauda walieleza Sombetini walieleza Sakina. Waliulizwa swali lolote  kukanusha kuwa haya maeneo hayopo ndani ya  jiji la Arusha

 

SABAYA: Ndiyo lipo

 

Baada ya Hakimu Dkt Kisinda Kuingia Kwenye chumba cha mahakama na mawakiki wa pande zote mbili kujitambulisha.

 

Hakimu akamueleza Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya kuwa Mahakama inamkumbusha kuwa bado yuko chini ya Kiapo azingatie Kusema ukweli.

 

Akiwa mbele upande wa  kizimba cha kulia Sabaya akaanza kujibu maswali.

 

Sehemu ya maswali ya dodoso ya mawakili wa serikali na majibu ya Sabaya.

 

 

Wakili Neema Mbwana

 

 

WAKILI:Ukiongozwa na wakili Mahuna ulisema una ndoa ulioa lini na ulimuoa nani 

 

SABAYA: nilifunga ndoa tarehe 15.7.2018 na nilimuoa Jesca Thomas na ndoa yao ilifungiwa katika kanisa la Central Sabbath Church. Wasiamizi wa ndoa Elibariki Nko na mama Ruth Urassa

WAKILI: Umeleta hati yoyote kuthibitisha kuwa umeoa 

SABAYA:Kwenye hati ya mashitaka hakuna sehemu inayolalamikia ndoa yangu

WAKILI:Umeleta uthibitisho hapa mahakamani

SABAYA:Ndio uthibitisho ni Mimi hapa mume wake 

WAKILI:Umeleta uthibitisho wa maandishi wa cheti hapa mahakamani

SABAYA: Sijaleta lakini Mimi ndie mume wake na ndo ushahidi wenyewe

 

WAKILI:kwajinsi ulivojieleza ulieleza kuwa ulikuwa mteule wa Rais na Jinsi ulivyojieleza ulisema uliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya 

SABAYA:Ndio

WAKILI: Ulikula kiapo cha ukuu wa wilaya

SABAYA:Ndio

WAKILI:Kama uliapa unakubaliana na Mimi kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria 

SABAYA:Upo sahihi

                 

WAKILI:Unafahamu kuwa dhima ya umilikiji wa laini ya simu ni swala la kisheria 

SABAYA:Ndio nafahamu

 

 

WAKILI:0758707171 nakumbuka namba hiyo ilizungumziwa hapa mahakamani 

SABAYA:Nakumbuka 

WAKILI:Na namba hiyo ilikuwa na Usajili wa Lengai ole Sabaya 

SABAYA:Ni sahihi nakumbuka 

 

WAKILI: Mheshimiwa naomba kielelezo cha tatu upande wa jamhuri akampatia shahidi ni taarifa ziilizo wasilishwa mahakamani na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom 

 

 WAKILI: Hiyo picha iliyopo hapo ni yanani Kwenye hiyo karatasi 

 

SABAYA:Ni picha ya inayofanana na Muonekano Wangu

 

WAKILI:Naomba usome maelezo yaliyopo hapo chini 

 

 

Sabaya: Namba hiyo ya simu imesajili na kumilikishwa kuwa Lengai Ole Sabaya .

 

WAKILI: Si ni kweli kwamba wewe kama mkuu wa wilaya ya Hai ulikuwa maarufu ulikuwa unafahamika na watu wengi

SABAYA:Hapana Mimi Sikuwa maarufu 

WAKILI:Samahani naomba kubadilisha swali

 

Wakili:Wewe ulipokuwa Mkuu wa wilaya mteuliwa wa Rais si ni kweli wananchi wengi walikuwa wanakufahamu

SABAYA:Sio kweli 

 

WAKILI:Unaweza kututajia namba ya ufungwa 

SABAYA:Namba ya ufungwa 

WAKILI:Unaweza sababu zilizopelekea wewe kuwa Mfungwa 

SABAYA:Hiyo sababu bado ipo mahakamani za juu inayobishaniwa mimi kuitwa mfungwa 

 

 

WAKILI:Mheshimiwa naomba kumpa wakili mwingine aendelee.

 

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU,  Jacopiya 

 

 

WAKILI:Ni kweli kwamba uteuzi wako ulitenguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

SABAYA:Sikutenguliwa nilisimamishwa kazi

WAKILI:Ni kweli kwamba ulisimamishwa kazi kwa ajili ya kupisha tuhuma zilizokuwa zinakukabili.

SABAYA:Sikuwa na tuhuma

 

WAKILI:Kwanini barua ya kukusimamisha kazi iliandika usimesimamishwa kupisha uchunguzi ulikuwa uchunguzi wa Afya.

SABAYA: Barua iliandikwa kupisha uchunguzi haikuandika tuhuma zozote.

 

SABAYA:Siwezi kuongelea maelekezo ya Mheshimiwa Rais hapa mahakamani

 

WAKILI:Unakubaliana na mimi kwamba uchunguzi uliosemwa uchunguzwe ndo matokeo ya kesi iliyokufikisha hapa mahakamani.

SABAYA:Sikubaliani maana hakuna uchunguzi uliofanyika 

 

WAKILI:Ni kweli Kwamba mbele ya Mahakama hii unashitakiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Sio kikundi chochote wala mtu binafsi au kikundi cha kisiasa

SABAYA:Sikubaliani na wewe

WAKILI:Unashitakiwa na nani 

SABAYA:Na waliotengeneza kesi hii

 

WAKILI: Mheshimiwa naomba hati ya Mashitaka na Kumapatia Sabaya Aisome.

 

WAKILI:Soma hapo juu hiyo hati ya Mashitaka imendikwaje

 

SABAYA:Republic dhidi ya Lengai ole Sabaya na wenzake

WAKILI:Kwahiyo hapo ni Jumhuri dhidi ya Lengai ole Sabaya  si ndio

SABAYA: Ndo unaniambia hapa kuwa Republic ndo Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lakini Kwenye hati hii imeandika neno Republic tu

 

WAKILI:Niwapi wameandikwa Kwenye hati ya mashitaka hao waliotengeneza hiyo kesi

SABAYA:Sijaona kama wameandikwa Kwenye hati ya Mashitaka

 

WAKILI:

SABAYA:Jamhuri haikutoa ushahidi waliotoa ushahidi ni Watu

 

WAKILI:Kuna kosa lolote mtu kuja kutoa ushahidi mahakamani 

SABAYA:Kunakosa ushahidi wa uongo

 

     

 

WAKILI: Simu namba 0758717170 ni kweli kwamba  Imesajiliwa kuwa majina yako 

 

SABAYA:Ndio imesajiliwa kwa jina langu

WAKILI: Iliwasiliana 0745978686 siku ya tarehe 22.1.2021 iliwasiliana na Mshitakiwa namba mbili

SABAYA:Sijui kwakuwa hiyo namba Sikuwa naitumia mimi

         

WAKILI:Mroso alisema kuwa tarehe 22.1.2021 mshitakiwa wa pili  na wa sita na wa saba walikuwepo kwa Mrombo

SABAYA:Sijui ushahidi wa huyo mtu aliousema 

 

WAKILI:Utakubaliana na Mimi kuwa mnashitakiwa kwa ushahidi na sio muujiza 

SABAYA:Sikubaliani na wewe na hakuna ushahidi wowote wa maana ulioteletwa kudhibitisha hilo.

      

WAKILI:Ukishakuwa mtuhumiwa unaweza kuchagua mahabusu

SABAYA:Kwa kufuata sheria sikulalamikia mahabusu nililalamikia jinsi sheria zilivyovunjwa

 

WAKILI:Ukiwa mtuhumiwa una haki ya kuchagua mahabusu maana ulisema hapa kuwa ukiwekwa Kwenye mahabusu ya Takukuru

SABAYA:Nilalamikia kuwekwa mahabusu siku nane bila kuhojiwa wala Kusikilizwa.

WAKILI:Ukieleza mahakamani kuwa ulipokamtwa ulipelekwa kwenye mahabusu ya TAKUKURU na siyo polisi.

SABAYA:Ndio

 

WAKILI:Swali langu sasa mtuhumiwa anaweza akachagua mahabusu upelekwe polisi na sio TAKUKURU

 

SABAYA: TAKUKURU hawana Mahabusu kwa Mujibu wa Sheria.

 

WAKILI:

SABAYA:Ndio Kwa Mujibu wa Sheria

WAKILI:Sheria Gani

SABAYA:Kwa mujibu wa sheria nilitakiwa kupekekwa polisi na sio mahabusu za TAKUKURU.

WAKILI:Kwa Sheria ipi na kifungu kipi

SABAYA:Mh hakimu Hilo ndo jibu langu

 

 

WAKILI:Kunasheria yoyote ile inayokataza uchunguzi kumkamata mhalifu mahali popote

SABAYA:Nililalamikia kukaguliwa usiku bila kibali cha kisheria na sheria hairuhusu kukaguliwa usiku bila kufuata taratibu za kisheria.

 

WAKILI:Nikweli kwamba pamoja na kulalamilia namna ulivyokamatwa

 

 

WAKILI:Hauwezi kutoa uahalali kwa kufanya uharamu inawekezana mnanitendea uonevu ndiyo maana mnapita ‘short cut’ kwa kuvunja sheria

 

Wakili:Nikweli kwamba katika watuhumiwa wote ni wewe pekee ulikuwa mtumishi wa umma 

 

 

SABAYA: Sifahamu hao wengine kama walikuwa watumishi wa umma maana siwafahamu.

 

WAKILI: Mheshimiwa naomba kupatiwa hati ya mashitaka

WAKILI:Kwamujibu wa hati ya mashitaka ni wewe tu ndiyo uliyeandikwa kuwa ni mtumishi wa serikali

SABAYA:Kwa Mujibu wa hati ya mashitaka ni kweli imeandika hapa nini Mimi peke yangu nilikuwa mtumishi wa serikali.

 

WAKILI:Kwa Mujibu wa hiyo hati ya mashitaka ni wewe tu uliyekuwa na madaraka

SABAYA:Ni kweli nilikuwa na utumishi wa Umma na sio madaraka kwa mujibu wa hati hiyo.

 

WAKILI:Ni kweli kwamba kwa huo utumishi wa umma ulikuwa ni Mkuu wa wilaya

SABAYA:Nilikuwa Mkuu wa wilaya ya Hai

Wakili:Sikweli kwamba ulikuwa na Mamlaka na Madaraka 

SABAYA:Ndio Nilikuwa na Madaraka

WAKILI:Na Mamlaka

SABAYA:Mamlaka ni Jibu Lako

WAKILI:Nikweli kwamba Kwenye hati ya mashitaka haijaeleza kuwa watuhumiwa wengine hawana Madaraka na Mamlaka

 

SABAYA : Mheshimiwa hakimu wakili aeleze kama anajibu kutoka na hati ya mashitaka au anataka majibu yangu kama Lengai Ole Sabaya

 

Wakili akafafanua kuwa anauliza kutokana na Hati kutokana na Shahidi kuitambua hati hiyo 

 

Sabaya akajibu kuwa yeye hafahamu

 

WAKILI:Kwa kuwa wewe ulikuwa pekee ndo mwenye Madaraka ni sahihi kuwa uliyatumia Madaraka yako vibaya

SABAYA:Utakuwa hapo sahihi

0 Comments:

Post a Comment