ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya
ya Hai, Lengai Ole Sabaya amedai kuwa hakuona CCTV video zilizoonyesha eneo la
ukumbi (hall) ndani ya benki ya CRDB tawi la Kwa Mrombo zilizotolewa na
kupokelewa kisha zikaonyeshwa mahakamani hapo kwa kile alichodai aliona 'movie'.
Ametoa majibu hayo leo mbele
ya hakimu Mkazi, Patricia Kisinda wa mahakama ya wilaya ya Monduli
anayesikiliza shauri hilo kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Arusha wakati
akiulizwa maswali ya dodoso na wakili wa serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia.
Sabaya ambaye katika hatua
za awali alidai hakuiona kabisa video hiyo lakini wakili wa Serikali alipozidi
kumbana huku akimkumbusha kuwa video hizo zilionyeshwa kwa nyakati tofauti na
shahidi wa nane wa Jamhuri, Johnson Kisaka na
shahidi wa 10 Fransis Mrosso ndipo akakiri kuona 'movie'.
Sehemu ya mahojiano hayo
ni kama ifuatavyo
WAKILI:alikuja shahidi
wa 10 Mrosso akadai kuwa bwana Macha (Jackson) alikuwa amevaa tisheti ya
mistari
SABAYA: alieleza
hivyo
WAKILI: Kwenye CCTV
video za benki ya CRDB bank hall uliziona
SABAYA:Sikuziona
WAKILI: CCTV video
za CRDB kwa mrombo zikichezwa hapa mahakamani hukuona
SABAYA: Sikuona
WAKILI: Wakati
zikichezwa ulikuwa umelala?
SABAYA: Nimesema
sikuziona
WAKILI:Zilipoletwa kwa
mara ya kwanza na shahidi wa nane wa Jamhuri Johnson Kisaka hapa uliziona
SABAYA: Sikuziona
niliona movie.
WAKILI: Vilevile alikuja
Mrosso zikachezwa kuanzia saa 10.04 mpaka 11.15 uliziona hukuziona
SABAYA:sikuziona
Wakili wa serikali
Mwandamizi, Felix Kwetukia akimhoji Sabaya maswali ya dodoso
Wakili:Suala la usajili
wa simu liko kisheria na si kwa matakwa ya mtu binafsi
Shahidi: Ndiyo
nakubali
Wakili: Unakubaliana
na mimi sheria ya usajili inaweka vifungu hususani kifungu namba 12, moja
sheria inakataza kuazimisha laini za simu.
Shahidi. Sikubaliani
Wakili : Kwa wewe
uliyekuwa na dhamana ya kuilinda na kutetea sheria unakubaliana kuwa hairuhusiwi
kuazimisha laini ya simu
Shahidi: Unaweza
kuiazimisha kwa mtu
Wakili: kwa sheria ipi
Shahidi: Sheria hiyo
inatoa masharti
Wakili: Wewe ulikuwa na
dhamana ya ukuu wa wilaya ukasajili line ya simu kwa kitambulisho cha NIDA
halafu ukaiazimisha kwa mtu mwingine
Shahidi: Inaweza kwa
mujibu wa sheria
Wakili: Sheria gani
inayosema hivyo
Shahidi: Katika sheria
ya mawasiliano
Wakili:
Nilikusikia ukisema kuwa bwana Ramadhani Juma alikuja gerezani akawashawishi wenzako watoe maelezo ya
kukukandamiza wewe anajua kwa namna gani atawatoa kwenye kesi mahakamani
Shahidi: Ni kweli
Wakili: Ramadhani
alikuja hapa alitoa ushahidi wakati akitoa ushahidi aliulizwa maswali ya dodoso
mawakili wako walimuuliza juu ya hilo
Shahidi: Aliulizwa na
mawakili wawili
WAKILI: Kuna swali lolote
bwana Ramadhani Juma aliulizwa juu ya utetezi wako kuwa alijua atafanyaje huko
mbele mahakamani namna ya kuwatoa watuhumiwa wengine mahakamani hapa kwenye
kesi
SABAYA: Aliulizwa
WAKILI:alikuja bwana Ramadhani
Juma kuna swali lolote aliloulizwa juu ya mkataba wa gari baina yako wewe na Oilcom
wa ununuzi wa gari kwamba alikabidhiwa na bi Jesca
SABAYA: Aliulizwa
WAKILI:Unatambua kwamba
mahakama ni chombo huru
SABAYA:Natambua
WAKILI:Unatambua
mahakama katika kutenda wajibu wake wa kutoa haki haiingiliwi na chombo
chochote cha dola
SABAYA: Haipaswi
kuingiliwa
WAKILI:Kwa hiyo
unakubaliana na mimi kwamba Ramadhani Juma hana uwezo wala mamlaka kuingilia mahakama
katika utendaji wake
SABAYA: Hana
WAKILI:Alikuja shahidi
namba 11 Bw Shabani katika ushahidi wake alisema aliwakuta wewe pamoja na
mshitakiwa wa pili, wa tatu, wa tano pamoja na mke wako ndiyo alivyosema hapa
mahakamani
SABAYA:Ndiyo alisema
hivyo
WAKILI: Wakati akitoa
ushahidi hapa mahakamani aliulizwa kuwa aliwakamata nyie wanaume wanne na
mwanamke mmoja mkiwa sehemu moja
SABAYA:Aliulizwa
WAKILI: Kuna swali
lolote aliloulizwa la kukanusha kuwa aliwakamata wewe mtuhumiwa namba mbili,
tatu, na tano silvester pamoja na mkeo mkiwa mahali pamoja
SABAYA: Aliulizwa na
akakanusha
WAKILI:Alikuja bwana
Sabri shahidi namba 12 pamoja na ushahidi wake wote alituletea mkataba wa gari
kuna swali lolote aliulizwa hapa juu ya sahihi na jina lako
SABAYA: ndiyo aliulizwa
WAKILI: nasema
specifical jina na sahihi yako
……
WAKILI: Bwana Lengai
narudi nyuma kidogo kuwa uliazimisha namba ya simu, huko nitarudi baadaye
kidogo, unafahamu mahakama inaweza
kumkuta mtu hatiani hata kwa kosa ambalo haliko kwenye hati na mashitska
SABAYA: Nafahamu
WAKILI:Hadi sasa hivi
hakuna uthibitisho uliotoa wa maandishi kutoka vodacom ulioleta hapa mahakamani
kuwa laini ya simu uliyoisajili inatumiwa na mtu mwingine
SABAYA: Sijawasiliana na
vodacom
WAKILI: Na hata
alipokuja shahidi bwana James Wawenje toka vodacom hakuulizwa swali lolote juu
ya namba yako uliyosajili kwa kitambulisho chako cha nida inatumiwa na mtu
mwingine
SABAYA:Aliulizwa
WAKILI:Nasema hii namna
0758707171 alithibitisha inatumiwa na mtu mwingine hii namba iliyosajiliwa kwa
kitambulisho chako na particulars zako inatumiwa na mtu mwingine
SABAYA: Hajaulizwa
manake yeye alileta ushahidi wake
WAKILI: Kaulizwa
hajaulizwa
SABAYA: Hajaulizwa
WAKILI: Una kubaliana na
mimi kwamba jambo moja kwenye kesi si lazima lithibitishwe na mashahidi 20
SABAYA: Uliiza swali
vizuri
WAKILI: Uliulizwa kuwa
mtu haufungwi kwa kuleta mashahidi wengi
SABAYA:
WAKILI: Shahidi mmoja
anaweza kuthibitidha jambo linalobishaniwa
SABAYA: Mh kama ni swali
la Ngemela naomba nijibu kwa jibu nililojibu
WAKILI: Jambo moja
katika kesi linaweza kuthibitishwa na shahidi mmoja na si lazima kuleta
mashahidi lukuki
SABAYA:Sijaelewa
alipoulizwa mara ya pili akasema inategemea quality ya mashahidi
WAKILI: Jibu swali langu
unaweza au hawezi
SABAYA:
WAKILI: Alikuja shahidi
namba 10 Mrosso na 13 Ramadhani Juma wakawatambua Mrosso aliwatambua watu
aliokuwa nao kule benki miongoni mwao akiwemo Macha (Jackson) na alimshika
bega hapa makahamani
SABAYA:Macha yupi
WAKILI:Mshitakiwa namba
sita na wewe pia alikushika bega
SABAYA:Ndiyo
WAKILI:Akadai kuwa bwana
Macha alikuwa amevaa tisheti ya mistari
SABAYA: Alieleza
hivyo
WAKILI: Kwenye CCTV za CRDB
Kwa Mrombo eneo benki hall ulizona hapa mahakani
SABAYA:Sikuziona
WAKILI:CCTV za CRDB Kwa Mrombo zikichezwa hapa mahakani
haukuona
SABAYA:Sikuona
WAKILI: Wakati
zikichezwa ulikuwa umelala
SABAYA: Nimesema
sikuziona
WAKILI:Zilipoletwa kwa
mara ya kwanza na Johnson Kisaka hapa mahakamani uliziona
SABAYA: Sikuziona
niliona ‘movie’
WAKILI: vilevile alikuja
Mrosso zikachezwa kuanzia saa 10.04 jioni mpaka 11.15 jioni ulizona
hukuziona
SABAYA:Sikuziona
WAKILI: Uliongea hapa
juu ya kutoletwa cheti cha seizure hapa mahakama kunaondoa ukweli kwamba ile
gari imekamatwa
SABAYA: Inaondoa
WAKILI:Inaondoa ukweli
kuwa ile gari inashikiliwa PCCB mpaka likaletwa hapa mahakamani
SABAYA:Inaondoa ndiyo
inaondoa
WAKILI:Katika hilohilo
alikuja bwana Shaban akaeleza kuwa yeye ndiyo alikamata lile gari T 222 BDY 25/
5/ 2021 na akaliendesha mpaka ofisi za PCCB upanga ulimsikia iz akisema hivyo hapa
mahakamani
SABAYA: Hakusema hivyo
……
WAKILI:Katika ushahidi
wako ulisema kuwa Mrosso hakuwa katika
position hivyo asingeweza kujaza magari yanayoingia na kutoka kwani hata magari
yakitoka akiwa chini ya ulinzi
SABAYA: Hayo si maelezo
yangu ya ushahidi
WAKILI: Ulimsikia bwana Marandu
akisema yeye ndiyo alikuwa akijaza kile kitabu
SABAYA:Sikumsikia kwa
sababu
WAKILI: Baasi haukumsikia,
vilevile kuna maswali uliulizwa na wenzangu ni kweli ulisimamishwa ukuu wa
wilaya ili kupisha uchunguzi
SABAYA: Ni sahihi
WAKILI: Polisi wana
kitengo cha uchunguzi kiko chini ya DCI
SABAYA: Sahihi
WAKILI: Unakubaliana na
mimi polisi wanachunguza makosa ya jinai
SABAYA:Nakubali
WAKILI: Na TAKUKURU ni
chombo cha uchunguzi
SABAYA: Kinachohusu
makosa ya rushwa
WAKILI:Ni kweli kwamba
hadi sasa hakuna shahidi yeyeto kutoka polisi aliyekuja kutoa ushahidi kwenye
kesi hii
SABAYA: Hakuna
WAKILI: Kwenye ya jinai
namba 105/ 2021 ambayo imekwisha na na hii economic case na 272021 inayoendelea
SABAYA:sahihi
WAKILI: ni kweli kwamba
kesi namba 105 2021 ilipelelezwa na polisi
SABAYA: Hakuna mtu
alinihoji
WAKILI: Ni kweli kwamba
hakuna mtu hata mmoja wa TAKUKURU akihusika na hiyo kesi.
SABAYA: Mheshimiwa hayo
mambo yanabishaniwa mahakamani hivyo siwezi kuzungumza
WAKILI: Katika kesi
inayoendelea hadi tunafunga ushahidi hakuna afisa kutoka polisi aliyefika
isipokuwa watu watatu wa TAKUKURU
SABAYA: Ni sahihi
WAKILI:Ni kweli kwamba
kwenye kesi namba 105/ 2021 uliopewa nafasi ya kujitetea ukiwa na mawakili wako
SABAYA: Hiyo kesi iko
mahakamani siwezi kuzungumzia
WAKILI: Kwenye kesi hii
inayoendelea umepewa haki ya kusikilizwa na kujitetea ukiwa na mawakili wako
SABAYA: Ndiyo nimepewa
haki ya kusikilizwa
WAKILI: Wakati bwana
mrosso akitoa ushahidi wake hapa mahakamani ni kweli kwamba wewe ulielekeza kuwa
toa milioni 90 vinginevyo tuondoke wewe
SABAYA: Siyo kweli
WAKILI:Ni kweli kwamba
kwa mujibu wa CCTV footage ambazo wewe unasema huzijui mnamo au tuliache kwanza . Hivi kweli mtu mmoja
anaruhusiwa kuwa na mitandao ya makampuni yote
SABAYA: Anaruhusiwa
WAKILI: Na ukweli kwa mujibu
wa CCTV footage ambazo unasema huzijui kuanzia saa 10 43 mpaka saa 10 45 mtu
aliyetambuliwa na Mrosso kama Macha alikuwa anaongea na simu
SABAYA: Siitambui hiyo
CCTV
WAKILI: Unajua au haujui
SABAYA: mh hakuna CCTV iliyoletwa hapa mahakamani
WAKILI:Ulisema mshitakuwa
wa sita (Silvester Nyegu) hakuwa wakala wako kukupokelea fedha
SABAYA: Mh nilikuwa
najibu swali la Ngemela (Wakili wa utetezi)
WAKILI:Shahidi wa 10
alikuja hapa akasema ulimkabidhi vijana wawili ili waende CRDB tawi la kwa Mrombo ili wakalete hela
SABAYA: Hakusema
unaongeza maneno
WAKILI: Ni kweli kwamba
bwana Mrosso alitoa ufafanuzi wa kukosewa kwa akaunti yake hapa mahakamani
SABAYA: Hakutoa
WAKILI:Uliulizwa swali
hapa jana ukajibu hapa hujui juu ya bwana Mrosso
……
WAKILI: nitamuuliza
swali kutokana hati ya mashitaka Kuongoza matendo ya uhalifu, matendo ya rushwa,
matumizi mabaya ya madaraka katika mashataka haya lipo hilo la kisiasa
SABAYA: Mashitaka ni ya
kisiasa hilo ndiyo jibu langu
Mheshimiwa yangu ni hayo,
mengine Janet ataendelea
Wakili wa serikali
mwandamizi, Janet Segule
WAKILI: Sabaya habari ya
kwako pole sana nina maswali machache kama hatutazungushana katika kujibishana
. Umesema ulikuwa dc hai
SABAYA:Kweli
WAKILI: Nitakuwa sahihi
nikisema wakati ukipata uteuzi huo kuna watu wengine waliteuliwa kuwa maDC
SABAYA: Sahihi
WAKILI: Nitakuwa sahihi
nikisema kuwa katika maDC mliochaguliwa kwa kipindi chako ni wewe pekee
umefunguliwa mashitaka mawili na moja
unatumikia kifungo
SABAYA:Sifahamu
WAKILI: Vilevile umeeleza
mahakama kuwa ulisimamishwa ili kupisha uchunguzi
SABAYA:Aliyenisimamisha
ndiyo anaweza kujua hilo siwezi kumsemea mh Rais.
WAKILI: Ulidai kwamba
kwenye mkataba wa gari ulioletwa na shahidi wa 12 na ulipokelewa bila pingamizi
SABAYA: Wakati mkataba
unaletwa haikuwekwa pingamizi
WAKILI:Haikuwekewa
SABAYA: Nilisema mkataba
ule sio wa kwangu sikufanya nao manunuzi
WAKILI:Vilevile ukasema
kwamba kwa nini jina lako limetokea kwenye mkataba huo na sahihi si ya kwako
SABAYA: Nilisema
kuwa
WAKILI:Ni sahihi kuwa
mahakama ndiyo inachambua kijua uhalali wa ushahidi uliotolewa mahakamani
SABAYA:Mahakama ndiyo
inauchambua
WAKILI:nikurudishe kwa
mshitakiwa namba tano ulisema kuwa ulikuwa unamuona kama sehemu ya watumishi wa
wilaya ya hai
SABAYA: Kama sehemu ya
watumishi
WAKILI: Shahidi namna 12
Sabri katika ushahidi wake mahakamani alisema kuwa wakati mkiuziana gari mshitakiwa
namba tano alikuwa eneo la black wood
SABAYA: Alisema hivyo
WAKILI: Shahidi huyo
alisema kuwa alishakutana na wewe pamoja na mshitakiwa huyo katika mkutano mkuu
Dodoma
SABAYA: Hakusema kwenye
mkutano mkuu
WAKILI:Kwenye mkutano wa
CCM
SABAYA:Hakusema kwenye
mkutano wa ccm
WAKILI:Na madai yote
hayo ya kusema ya kukutana na mshitakiwa namba tano pamoja naye Black Wood
pamoja na Dodoma hakuulizwa maswali
SABAYA: Aliulizwa
WAKILI:Mkataba ulioletwa
na Sabri ambacho ni mkataba wa mauziano ambapo kuna namba (anazitaja namba za
simu mbili) .... ulisema siyo ya kwako
SABAYA:Ndiyo nilisema si
ya kwangu kwani tayari wameleta kielelezo kina namba nyingine.
WAKILI: Walisema wakati
ukikamatwa ulikamatwa ulikuwa na namba mbili tofauti 0714 038888 0754 585458
SABAYA: Ndiyo na
nilizitaja
WAKILI: Sasa Lengai nitakuwa
sahihi nikisema kwamba si ajabu mtu kuwa namba zaidi ya moja na sheria haikatazi
SABAYA: Kuwa specific ni
sheria au …… mimi nina namba mbili
WAKILI: Nitakuwa sahihi
kuwa sheria haikatazi
SABAYA: Haikatazi
WAKILI: Hivyo ungeweza
kuwa na zaidi ya hizo mbili
SABAYA: Nisingeweza
ndiyo sababu ninazo hizo mbili tu
WAKILI:Kwenye count
(shitaka) ya tano inahusiana na utakatishaji wa fedha ulidai kwamba unashangaa
gari linadaiwa kunuliwa tarehe 2/ 2/ 2021 wakati hati ya mashitaka inakutuhumu
kutakatidha fedha wakati hati ya mashitaka inakutuhumu kutakatisha fedha 22/ 1/
2021 ulisema hivyo
SABAYA: Nilisema hivyo
WAKILI:Ni sahihi kwamba
22/ 1/ 2021 unayodaiwa kutakatisha fedha unazodaiwa kama rushwa kutoka kwa Mrosso
na kuitakatisha ni tarehe kabla ya tarehe 2/ 2/2021 uliyodaiwa kutakatisha
fedha
SABAYA: Sahihi
WAKILI: Katika ushahidi
wako ulisema kuwa Mrosso alijaza kitabu cha wanaoingia na kutoka mbele ya afisa
wa TAKUKURU
SABAYA: Nilisema alijaza
walipofika maafisa wa TAKUKURU
WAKILI: Ulikuwepo
SABAYA: Hayo ni maelezo
ya shahidi wa tatu wa jamhuri
WAKILI: Ok kwa maelezo
yake. Nitarudi kwa mke wako shahidi namba mbili wa utetezi Jesca ni sahihi
alisema kwamba aliwasiliana na broker (dalali) huyo wa mazao majira ya saa nane
mchana na baada ya hapo hawakuwasiliana tena
SABAYA: Alisema
walifanya mawasiliano
WAKILI: Wewe ulimsikia
akisema kwamba alifanya mawasiliano na dalali majira ya saa nane mchana
SABAYA: Alikuwa anajibu
swali alisema alifanya mawasiliano saa nane na akasema alifanya mawasiliano
baadaye na ipo kwenye ushahidi
WAKILI: Sabaya ni sahihi
kwamba shahidi wako wa pili Jesca akitumia simu yako namba ...
SABAYA: Alisema kuwa
siku hiyo 22/ 1/ 2021 alisema alikuja Arusha na majira ya usiku alirejea Hai
SABAYA: Sahihi
WAKILI: Alisema kuwa
wakati akielekea Kisongo alipita Mbauda
SABAYA: Ni sahihi
alitaja na maeneo mengine alisema kuwa pia anafanya biashara Mbauda
WAKILI: Na aliporudi
alipita Majengo, Tripple A Mianzini wakati akielekea Hai
SABAYA: ni sahihi
aliyataja
WAKILI: mh naomba
kielelezo namba 3 Jesca alisema alikuwa anatumia simu 0758707171
kuwasiliana na watu
SABAYA: Hakusema
alitumia hiyo tu na simu nyingine aliyokuwa nayo kwa mambo binafsi
WAKILI: Ana mambo
binafsi
SABAYA: Kabisa
WAKILI: Alisema ni saa
ngapi alipita Mbauda kuelekea Kisongo
SABAYA: Sikumbuki saa
WAKILI: Sabaya naomba
nikupatie kielezo namba tatu katika maelezo shahidi wa pili wa utetezi ambapo
alisema alifanya mawasiliano na dalali kuanzia saa nane mpaka saa nne na dakika
8 usiku wa siku hiyo ya tarehe 22/ 1/ 2021 kuna sehemu yoyote unasoma Majengo
SABAYA: Mh sijui mnara
unaosoma Majengo mimi siwezi kujua mnara unaosoma Majengo
HAKIMU Janet kuwa
specific
WAKILI: Akarudia
swali
SABAYA:Mh hakimu hiyo
itanipa shida kujibu labda kama anahitaji maoni yangu
HAKIMU Amekuuliza kwenye
kielelezo kuna sehemu inasoma Majengo
SABAYA:Hakuna sehemu
inasoma Majengo kwa mujibu wa kielelezo hicho
WAKILI: Kuna sehemu
yoyote inayosoma Kisongo
SABAYA: Kwa mujibu wa
kielelezo hicho hakuna
WAKILI:Lengai embu
ikumbushe mahakama siku hiyo mke wako alirejea Hai saa ngapi
SABAYA: Usiku
WAKILI: Saa ngapi
SABAYA: Sikumbuki
nilikuwa nimelala
WAKILI: Kwa mujibu wa
kielelezo hiki namba tatu siku hiyo ya tarehe 22/ 1/ 2022 simu hii iliendelea
kusomeka ikiwa arusha mpaka tarehe 25 /1 /2021
SABAYA: Mheshimiwa kwa mujibu wa kielelezo simu hii ilisomeka
ikiwa Arusha
Mh ni hayo tu kwa
shahidi naomba kurejesha kielelezo namba tatu.
Wakili wa utetezi, Moses
Mahuna tuko tayari kuendelea na re examination kulingana na muda wa mahakama
lakini kama muda hauruhusu tuko tayari kuendelea siku nyingine itakayopangwa na
mahakama.
Hakimu Kisinda, basi
tutaendelea jumatatu
0 Comments:
Post a Comment