MAJALIWA AMWAGIZA SIRRO KUWASIMAMISHA VIGOGO WA POLISI MTWARA NA KILINDI KUPISHA UCHUNGUZI

 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mikoa ya kipolisi ya Mtwara na Kilindi wakiwemo RPC na RCO ili kupisha uchunguzi wa mauaji yaliyotokea maeneo hayo.

Aidha ameunda Tume Huru ya Kiuchunguzi  itafanya kazi kwa siku 14 kuanzia kesho Jumamosi Februari 5,2022.

Hatua hiyo imetokana na  agizo la Rais, Samia Suluhu Hassan kutoa agizo la kuundwa tume huru tofauti na tume iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Maagizo haya yanakuja baada kifo cha mfanyabiashara wa madini aliyekuwa na umri wa miaka 25, Musa Hamisi mkazi wa wilaya ya Nachingwea mkoa jirani wa Lindi.

Inadaiwa kabla ya kuuawa alikamatwa na askari wa polisi Oktoba 20, mwaka jana akiwa katika nyumba ya kulala wageni Mkoani Mtwara akituhumiwa kuwa mwizi wa pikipiki na kufikishwa kituo cha poilisi kwa ajili ya mahojiano.


0 Comments:

Post a Comment