MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imemeliza kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote kwenye rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengao Ole Sabaya na wenzake wawili ambapo imepanga kuitaja Machi 15, mwaka huu kwa ajili ya kupanga tarehe ya uamuzi.
Aidha Mawakili wa Serikali, wameiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja zote 14 za rufaa zilizowasilishwa na mawakili wa waleta rufaa kwani hazina msingi kisheria huku wakisisitiza kuwa Sabaya kwenye ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa alifika kwenye eneo la tukio.
Pia wameeleza kuwa hakimu alifanya uchambuzi wa kina wa ushahidi wa mashahidi na vielelezo na kutoa huku na adhabu inayostahili kwa mujibu wa sheria kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na jeshi la polisi wakati wa upelelezi.
Jaji Sedekia Kisanya wa mahakama Kuu Kanda ya Musoma anayesikiliza rufaa hiyo namba 129/2021 kwenye mahakama Kuu Kanda ya Arusha alipanga tarehe hiyo baada ya kusikiliza hoja za rufaa kutoka kwa mawakili wa waleta rufaa na majibu kutoka kwa mawakili wa serikali ambao ni wajibu rufaa na hoja za nyongeza kutoka kwa mawakili wa waleta rufaa.
Kwenye rufaa Sabaya na wenzake Silvester Nyengu na Daniel Mbura wanaiomba mahakama kuwafutia hukumu na adhabu waliyopewa ya kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambayo hakimu katika uamuzi wake kwenye shitaka moja aliwatia hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa makundi iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi Arusha.
Mawakili wa waleta rufaa wiki iliyopita waliwasilisha hoja 14 ikiwemo kuwa hakimu hakufanyia tathmini ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo katika kufanya uamuzi wake na kuwa polisi hawakufanya uchunguzi wao ipasavyo.
Leo mawakili wa serikali wakiendelea kutoa hoja zao za majibu ya rufaa kwa siku ya pili na kuiomba mahakama hiyo kutupa hoja za mawakili wa waleta rufaa kwa kile walichodai kuwa hazina msingi kisheria na kuwa haziingii kwenye msingi wa kesi.
"Kwa kupitia hoja tulizowasilisha ni kuwa mahakama ya chini ilifanya 'proper evaluation' na kufanya maamuzi sahihi na mahakama ilijielekeza kuangalia ushahidi wa msingi wa mrufani wa kwanza mpaka wa tatu (Sabaya, Nyengu na Mbura) ulizingatiwa na kwa nini waliunganishwa mahakama ilitimiza wajibu wake ipasavyo hatujaona mahali popote mahakama hii itaingilia ule uamuzi," alieleza Wakili wa serikali Baraka Mgaya na kuongeza.
"Tunaomba mahakama yako itupilie mbali sababu zote 24 zilizowasilishwa na kuzingatia hukumu na adhabu iliyotokewa na mahakama ya chini,".
Mgaya alieleza kuwa waleta rufaa wanadai ushahidi wa shahidi wa sita, Bakari Msangi usiaminiwe lakini katika kuangalia uaminifu wa shahidi unaangalia msimamo wa ushahidi alioutoa ukiulinganisha na ule uliotolewa na mashahidi wengine pamoja na wa mleta rufaa, Sabaya utaona shahidi alisema kweli.
Aliiomba mahakama hiyo kuzingatia ushahidi wa Shahidi wa sita, Bakari kuwa mleta rufaa wa kwanza , sabaya alikuwa kwenye tukio kwani hauna tofauti na ule uliotolewa na shahidi wa pili, Numan Jasin, shahidi wa tatu, Ramadhani Ayubu, Shahidi wa nne, Hajirin Saad Hajini, Shahidi wa tano, Msuya ambaye ni mmiliki wa duka la jirani aliyesema alimuona Mleta rufani wa kwanza, Sabaya akiingia dukani kwa shahidi wa kwanza Mohamed Asaad Hajirini.
" Mheshimiwa jaji habari aliyotoa PW 6 (Msangi) ukiangalia mwendelezo wake hauna tofauti na Mashahidi wa pili, wa tatu, wa nne na wanne wa Jamhuri na sehemu niliyokuwa naomba mahakama yako izingatie ushahidi wa shahidi wa tano wa jamhuri ambaye ni mmiliki wa duka la jirani ambaye anasema alimuona mleta rufaa wa kwanza majira saa 11 akiingia dukani kwa shahodo wa kwanza," ameeleza Mgaya na kuongeza
" Naomba mahakama yako izingatie na ushahidi wa mleta rufaa wa kwanza,(Sabaya) ambaye anakiri siku ya tukio alikuwa Arusha na akihitaji kumuinterrogate shahidi wa kwanza wa jamhuri Mohamed Saad Hajirini. Hivyo ukiangalia maelezo hayo utaona Sahihidi wa sita ni mkweli na hakuna sababu ya kumtilia mashaka,".
Mgaya alieleza mahaka kuwa kitendo cha mleta rufaa wa pili, Nyengu utofauti wake wa kile alichokubali kwenye usomaji wa maelezo ya awali (PH ) kuwa yeye ni msaidizi binafsi wa Sabaya na kile alichokuja kujitetea kwa kukana nafasi ni katika kujaribu kuonyeshz hana ukaribu nanmleta rufaa wa kwanza.
" Wakati wa PH alisema yeye ni msaidizi binafsi wa Sabaya baada ya ushahidi wakati akijitetea akasema yeye si msaidizi binafsi wa Sabaya.Huu ni uongo unaojaribu kujiweka mbali na mleta rufaa wa kwanza ili asionekane kuwa alikuwa kwenye tukio," alieleza Mgaya.
Wakili wa serikali Mwandamizi, Veridiana Mlenza alieza mahakama hiyo kuwa sheria na taratibu zote zilizingatiwa wakati wa kuwasomea waleta rufaa PH na hiyo inathibitishwa na hatua ya rufani hao na mawakili wao kusaini taarifa za warufani mara baada ya kusomwa mahakamani.
"Wanasema kuwa shahidi wa tatu wa jamhuri alisema fedha alizokuwa kuwa nazo zilikuwa kwa ajili ya kununua vitu vya nyumbani tumepitia mwenenendo hatujaona mahali amesema kuwa alienda kununua vitu hiki ni kitu kipya," alieleza wakili wa serikali mwandamizi Mlenza na kuongeza
"Wanasema shilingi 35,000 ingewezaje kununua neti lakini hili jambo linaibuliwa kwenye rufaa kwa sababu kwenye ushahidi wake kulingana na mwenendo alisema alienda kununua neti baada ya kupata mteja ambapo baada ya kuchagua neti kabla ya kwenda kulipa akawekwa chini ya ulinzi kwa amri ya mleta rufaa wa kwanza akasachiwa akanyang'anywa fedha zake na simu,".
Naye wakili wa serikali Mwandamizi, Ofmed Mtenga alisema hoja za upande wa waleta rufaa kuwa shahidi wa kwanza wa jamhuri aliieleza mahakama kuwa aliona tukio zima la januari 9, 2021 kupitia picha za Video za CCTV zilizokuwa dukani hapo si sahihi kwani kwenye ushahidi wake shahidi huyo ambaye ni mmiliki wa duka alieleza kuwa aliona tukio hilo kupitia kamera mbili tu kwani nyingine nne zilijuwa zimeelekezwa ukutani hivyo hazikuonyesha kitu.
"Suala la CCTV footage kwa nini hazikuletwa mahakamani ukiangalia ushahidi wa PW SEVEN (shahidi wa saba, Mpelelezi wa wilaya ya Arusha, Gwakisa Minga) alisema zilikuwa zimeingiliwa kwa maana ya kwamba kati ya sita mbili ziligeuziwa ukutani na nne zilikuwa zinaonyesha maeneo mengine hivyo zisingeisaidia mahakama," alieleza wakili wa serikali, Ofmed na kuongeza.
" Ukiangalia ushahidi wote wa PW 1 (Mohamed Saad Hajirini) alisema kuwa hata hakuweza kujua waliochukua fedha kwani kamera mbili tu ndiyo hazikuingiliwa sasa hata wenzetu hawakumuuliza wakati akitoa ushahidi wake endapo hizo kamera mbili zikuwa zinaelekea kaunta,".
0 Comments:
Post a Comment