DKT MWINYI AONGOZA KUAGA MWILI WA DK MWELE


RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi ameongoza waombolezaji viwanja vya Karimjee kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele katika Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Mwele Malecela aliyefariki nchini Uswizi mwishoni mwa wiki iliyopita.




Aidha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson nao walikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kuuaga mwili wa Dk. Mwele ambao umewasili usiku wa kuamkia leo Februari 19, 2022 ukitokea Geneva ambako umauti ulimkuta.




Akizungumza wakati wa kutoa salam za pole, Rais Mwinyi amesema; “Kwa muda wote ambao nimemfahamu Dkt. Mwele, kikazi alikuwa ni mtu wa kujituma sana ‘committed and very professional.


“Dkt. Mwele ameitumikia Nchi yake, sisi sote tunapaswa tujiulize endapo tutaweza kufikia yale ambayo ameyafikia na ukiacha upande wa kazi kama mtu alikuwa na utu mkubwa, alikuwa karibu sana na watu alikuwa anapenda kusaidia," .

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa amesema; “Nimekuja kutoa salamu za Rais
Samia Suluhu ambaye angependa kujumuika hapa kutoa pole amenituma nilete salamu za pole kwa familia kufuatia kifo cha mpendwa wetu Dkt. Mwele, amesema atakaporudi atakuja kukusalimia mzee Malecela,".

Baada ya kuagwa Karimjee, Mwili wa Dk. Mwele utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Dodoma kwa ajili ya maziko. 



Baada ya kuagwa Karimjee, Mwili wa Dk. Mwele utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Dodoma kwa ajili ya maziko.

0 Comments:

Post a Comment