TUME YA UMWAGILIAJI KUJENGA MABWAWA YA MAJI KILIMANJARO

Na Gifty Mongi, Moshi



TUME ya taifa ya umwagiliaji Mkoa wa Kilimanjaro imeanza kuchukua hatua kwa kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi sahihi ya maji kutokana na halo ya mabadiliko ya tabia ya nchi iliyopelekea maji kupungua katika baadhi ya skim


Mhandisi Said Ibrahim ni Meneja wa tume hiyo mkoa wa Kilimanjaro ambapo amesema hadi sasa hakuna athari za moja kwa moja ambazo zimeweza kujitokeza na kinachofanyika  ni kujipanga ili zisitokee na kuleta madhara.

Amesema hatua nyingine ni pamoja na kuziba mifereji ili kuepusha upotevu Wa maji lakini pia kujenga mabwawa ambayo yatatumika katika kuhifadhi maji ambayo yatatumika pindi kutakapokuwepo na uhaba Wa maji.



0 Comments:

Post a Comment