HIZI HAPA SABABU ZA TANZANIA KUWA NA SIMBA WENGI ZAIDI DUNIANI



TANZANIA imetajwa kuwa ni nchi yenye  nusu ya simba wote Duniani huku ikipongezwa kwa uhifadhi .

RAIS wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa, (SCI), Sven Lindqueast ameeleza hayo kwenye Mkutano wa 50 wa Mwaka wa Uwindaji wa Kitalii unaoendelea kufanyika jijini Las Vegas,  Marekani


Amesema kwa hatua hiyo anaipongeza Tanzania kwa juhudi kubwa za uhifadhi uliopelekea wingi wa wanyamapori hao.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  amesisitiza  kuwa nusu ya simba wote wapo Tanzania  kutokana na uimara wa Serikali  katika shughuli za  uhifadhi


Amesema kuimarika kwa shughuli za uhifadhi hususani kwa Wanyamapori walao nyasi ni moja ya sababu ya Tanzania kuwa na Simba wengi  hivyo imepelekea  Simba nao  kuongezeka kutokana na uhakika wa  chakula cha kutosha 


Dkt Ndumbaro amefafanua kuwa Simba hula wanyamapori walao nyasi na wanyamapori hao wamekuwa wengi kutokana na uwepo wa nyasi za kutosha  na usimamizi bora wa maeneo ya Hifadhi


" Kubadilishwa  mfumo kutoka wa kirai kwenda katika mfumo wa kijeshi kwa Watumishi wote wanaosimamia maeneo ya Hifadhi ni moja ya sababu ya simba kuongezeka kwa Simba nchini Tanzania" alisema Dkt.Ndumbaro


Waziri  Ndumbaro  amesisitiza kuwa Tanzania imefanikiwa kuwa simba wengi kutokana na Serikali kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini kwa kuitengea Wizara ya Maliasili na Utalii bajeti ya kutosha inayotumika katika kuendesha operesheni mbalimbali za kukabiliana na ujangili


Amesema Serikali imeweza kufanikiwa kukomesha tatizo la  ujangili kwa  zaidi ya asilimia 90 huku akisisitiza  kuwa inatarajia kumaliza kabisa tatizo la  ujangili  kufikia asilimia 100% ifikapo mwaka 2025. 


" Uthubutu wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan wa kuwa bega kwa bega na Wizara imekuwa chachu kwa Tanzania kuzidi kuongoza kwa kuwa na simba wengi Duniani"

https://www.instagram.com/p/CZId0Z8OS_z/?utm_medium=share_sheet

0 Comments:

Post a Comment