PROFESA NDAKIDEMI ATOA MIFUKO 50 YA SARUJI MVULENI


Na Gift Mongi, Moshi


MBUNGE wa jimbo la Moshi Vijijini,  Profesa Patrick  Ndakidemi  ametekeleza ahadi yake ya kuchangia mifuko hamsini ya Saruji iliyokuwa inalenga kuunganisha nguvu na wananchi wa vijiji vya Mji mpya na Mvuleni  vilivyoko kata ya Mabogini kwenye ujenzi wa zahanati itakayohudumia vijiji hivyo  viwili.



Prof Ndakidemi alikabidhi Saruji hiyo kwa mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni  kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wananchi  ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo kutoka kwa afisa mtendaji wa Kijiji hicho.






Aliwashauri wananchi kushiriki kikamilifu kwenye kuchangia ujenzi wa Zahanati hiyo kwani ikikamilika itapunguza kero ya wanakijiji kwenda mbali kupata huduma za tiba. 


Hafla hiyo  ilihudhuriwa na Diwani Wa Kata ya Mabogini Dr  Bibiana Masawe,  wenyeviti wa vijiji vya Mvuleni na Mji Mpya  pamoja na watumishi mbalimbali  wa serekali  na wakazi wa vijiji hivyo viwili.   


Kwa niaba ya kata ya Mabogini na wananchi wa vijiji vya Mvuleni na Mji Mpya, Mheshimiwa Diwani alimshukuru mbunge kwa mchango wake wa mifuko 50 ya  Saruji iliyokuwa na thamani ya shilingi laki saba na elfu hamsini (750,000).



Baaada ya kukabidhi Saruji, mbunge pia alitembelea eneo la ujenzi  na kujionea ujenzi unaoendelea


0 Comments:

Post a Comment