| Mtuhumiwa, Patrick Mmasy |
JESHI la polisi linamshikilia, Patrick Mmasi, (24) kwa tuhuma za mauaji ya mama yake, Ruth Mmasi, (40) ambaye anadaiwa mara baada ya kutekeleza mauaji hayo aliuficha mwili huo kwenye chemba ya choo ya nyumba yao iliyopo Njiro, Kontena, jijini Arusha.
Habari kutoka kwa ndugu ndugu wa marehemu zinadai kuwa mwili wa mfanyabiashara huyo wa madini ya Tanzanite umepatikana Desemba 24, 2021 baada ya polisi kufanya upekuzi wa kina kwenye nyuma hiyo aliyokuwa akiishi marehemu pamoja na mwanae.
Inaelezwa kuwa mtoto mwingine wa marehemu aitwaye, Patricia Mmasi (19) anayesoma nchini China, alipata mashaka akiwa China wakati alipojaribu kumpigia simu mama yake Ruth na simu yake kutopatikana kwa muda wote.
Alisema aliamua kusafiri kuja Tanzania kwa sherehe za Chistmass na kumuuliza kakaye Patrick kuhusu kutoonekana kwa mamayake na kutopatikana kwenye simu, ambapo kijana huyo alikuwa akimjibu kuwa kwani mama yako akiondoka huwa ananiaga? ndipo yeye na ndugu wengine wakaamua kutoa taarifa Polisi.
Aliongeza kuwa Polisi walipofika walifanya upekuzi katika sehemu mbalimbali za nyumba hiyo ya kisasa yenye gorofa moja na ndipo wakabaini mwili huo ukiwa ndani ya chemba la choo nyuma ya nyumba hiyo na mwili huo umegundulika zikidhaniwa kupita siku 14 ukiwa ndani ya chembe hiyo.
Ndugu huyo alidai kuwa marehemu alikuwa akiishi na kijana wake huyo ambaye ndiye Mtoto wake wa kwanza na mara nyingi walikuwa wakitofautiana .
Baadhi ya mashuhuda wa tukio Hilo wamedai kuwa mwili huo ulikuwa umeanza kuharibika na umehifadhiwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru Kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha (RPC) Justine Masejo alithibitisha polisi kumshikilia kijana huyo Patrick kwa tuhuma za kifo cha utata cha mama yake, marehemu Ruth Mmasi.
Masejo alisema wanamshikilia kijana huyo kwaajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakani.
Kwa Mujibu wa ndugu marehemu Ruth atazikwa nyumbani kwao kesho alasiri katika eneo la Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara.
0 Comments:
Post a Comment