SHIRIKA la Mtandao wa
mashirika ya Wafugaji, Wawindaji na Waokota Matunda nchini, (PINGOS), limewakutanisha
Maafisa maendeleo ya jamii, wakuu wa dawati ya jinsia ya polisi, maafisa ustawi
wa jamii, mshirika yasiyo ya Kiserikali, (NGO) wafugaji na wakulima kutoka mikoa
ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, na
Manyara.
Washiriki hao zaidi ya
30 wamekutana kwa siku mbili Wilayani Arumeru kwa lengo la kuweza kujadilia
namna bora ya kushirikishana maswala ya jinsia sanjari na kuhakikisha kuna
ushiriki mkubwa kwa kinamama katika swala la uongozi na utawala Bora.
Mkurugenzi wa shirika PINGOS,
Edward Porokwa akiongea na washiriki hao wakati akifungua mafunzo hayo amesema
anaamini mafunzo hayo yatasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia kwenye jamii
hizo.
Mafunzo hayo
yamewakutanisha washiriki zaidi ya 30
kutoka jamii za wafugaji kwenye wilaya
za Ngorongoro, Longido, mkoani Arusha na Hanang’ na Simanjiro mkoani Simanjiro
na Handeni Mkoani Tanga.
Amesema kuwa unyanyasaji
wa kijinsia imekuwa ukichangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwenye jamii huku
wanawake wakiwa hawapewi nafasi za uongozi kwenye jamii.
Afisa maendeleo ya jamii
wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni amesema kuwa vitendo vya ukatili kwenye
jamii ya wafugaji vimekuwa vikipungua kutokana na elimu shirikishi ambayo
imekuwa ikitolewa na serikali kwa kushirikiana na asasi za kiraia.
Ameelezea nafasi ya
mwanamke ya uongozi kwenye jamii ambapo amesema kuwa mfumo dume imekuwa
changamoto inayowanyima wanawake kuwania nafasi za uongozi
Porokwa amesema kuwa
wamegundua kuwa kuna mfumo dume kwa jamiii kutokana na iila na desturi mbaya
ndani ya jamii ambapo kinamama wamekuwa wakinyanyaswa huku wanaume wakipendelewa sana hivyo akawataka
washiriki hao kuangalia ni namna gani ya kuwatia moyo kinamama ili waweze kuwa
imara ndani ya jamii
Amesema kuwa changamoto
wanazokutana ni pamoja na uweke uwezo mdogo wa kinamama wa namna gani ya
kukabiliana na matatizo ya ukatili ya kijinsia, kukosa ushirikiano kwa wanaume
,na mwamko mdogo wa kinamama kushiriki Semina mbalimbali
Kwa upande wake afisa maendeleo
ya jamii kutoka Wilaya ya Longido Atuganile Chisunga amesema kuwa, matukio ya
unyanyasaji kijinsia kwa wanawake yamekuwa machache ukinganisha na zamani
kutokana na jitihada wanazozifanya za kutoa elimu na kuchukua hatua kali za
kisheria
Amesema kuwa, vitendo
vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikifanyika kwa kinamama, na watoto kutokana
na mila na desturi za wenyeji wa wilaya hiyo ambao ni Wamaasai jambo waliloamua
kukabiliana nalo kwa kuweka nguvu kazi ya kutoa elimu hasa kuwahamasisha wazazi
kuwapeleka watoto wa kike shule.
“Eneo la Namanga limekuwa
na changamoto ya malezi na makuzi kwa watoto kwani wanalelewa malezi ya
kunyanyaswa kwa kuwatumikisha watoto wao kazi ikiwa ni pamoja na swala la
vitendo vya kulawiti. Lakini kwa sasa hali imebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya
ofisi yangu kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kumua kutoa elimu
ya malezi na makuzi kwa wanajamii kuanzia ngazi ya mtaa,” anasema Chisunga.
Kwa upande wake afisa
maendeleo ya jamii wa wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni amesema kwenye wilaya hiyo vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimepungua ukilinganisha na miaka iliyopita.
“Mipango ya sera ya ulinzi
na usalama kwa watoto imesaidia sana pamoja na maafisa maendeleo ya jamii
kwenye ngazi zote kutokaa maofisini bali wanakwenda ndani ya jamii kupata
taarifa na kuendelea kutoa elimu ya kuwalinda wanawake na watoto wa kike na
ukatili wa kijinsia,” amesema Ngalisoni.
Hata hivyo ameiomba
serikali kuongeza maafisa maendeleo ya jamii ili wawe kwenye kila kata jambo
litakalosaidia kupunguza ongezeko la ukatili wa kijinsia ndani ya jamii hasa
kwa kinamama na Watoto.
0 Comments:
Post a Comment