WATALII 150 KUTOKA ISRAEL WAWASILI NCHINI


 
MKUU wa mkoa wa Arusha, John Mongela ameongoza mapokezi ya watalii 150 kutoka Israel wanaotembelea vivutio vya utalii vilivyopo kaskazini.

Watalii hao wamepokelewa leo Agosti 2, 2021 na kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, (KIA) baada ya kutua uwanjani hapo na ndege binafsi majira ya saa 10.30 alfajiri.

Mongela alisema kuwa utalii ni sekta ambayo ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Taifa ndiyo sababu Rais, Samia Suluhu Hassan  ametia mkazo kwenye uchumi akitaka ufunguke uwe wa kisasa zaidi. 

" Tutafanya kila linalowezekana kwa kushirikiana na 'agencies' zetu ambazo ndizo zinasimamia utalii TANAPA TTB na wengine kuhakikisha watu hawa wanaenda kuisimulia vema Tanzania na vivutio vyake," alisema Mongela.

Aidha aliipongeza Kampuni Uendeshaji na Uendelezaji  u
Uwanja wa KIA, (KADCO), uhamiaji na idara ya afya kwa kuweza kufanya kazi kwa weledi hivyo kutumia muda mfupi kukamilisha taratibu za kuwakagua na kuwapima afya watalii hao.

"Wamefanya kazi kubwa ya mfano ndani ya saa moja na nusu watu 150 wamekuwa 'cleared' nazipongeza mamlaka zote. Na wamezingatia tahadhari ya UVIKO 19 kwani watu wote hapa wamevaa barakoa watalii na tuliofika kuwapokea ni jambo jema sana," alisema Mongela.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya utalii nchini, (TTB), Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo alisema kuwa kwa mwaka huu hii ni awamu ya pili wanapokea watalii kutoka Israel ambapo awamu ya kwanza waliingia nchini Julai 27, mwaka huu nanilienda moja kwa moja Zanzibar.

Alisema kuwa kwa wanatarajia watalii wengine kutoka Israel ambapo watakuja kwa tarehe tofauti ambapo makundi mawili watatua KIA na kundi moja litatua Zanzibar hivyo kufanya idadi ya watalii hao kufikia zaidi ya 900 kwa mwaka huu. 


Kwa upande wake muongoza watalii kutoka kampuni ya Excelence guides, dereva, Silva Justine,  
alisema kuwa wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kutoa huduma iliyo bora kwa watalii hao kwani walipatiwa mafunzo maalum ya namna ya kujikinga na kuwakinga watalii wanapokuwa kwenye safari.

" Hapa ninahakikisho wote kwenye gari tumevaa barakoa na tuna vitakasa mikono na kama mnavyoona gari ina nafasi ya kutosha hivyo usalama kiafya kwa watalii na mimi upo wa kutosha," alisema.

Alisema kuwa safari hiyo ya siku nane inaanza hapohapo ambapo mata baada ya kutoka  KIA wanawapeleka wageni kupata kifungua kinywa Duluti kisha wanaelekea Tarangire halafu wataenda kulala Manyara.



 

0 Comments:

Post a Comment