Na Gift Mongi,Moshi
Uchakavu wa miundombinu pamoja na kukosekana kwa chanzo cha kuaminika cha nishati ya umeme katika kituo cha afya Mwika kikichopo kwenye jimbo la Vunjo kumesababisha utoaji wa huduma kutofanyika kwa kiwango stahiki kwa wagonjwa wanaoenda kupatiwa matibabu.
Hayo yameelezwa na mganga mkuu wa kituo hicho, Heriel Saria baada ya kupokeaa msaada wa shuka 50 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei ambapo pia ameeleza huduma zinavyotolewa chini ya kiwango kutokana na mazingira hayo kuwa chakavu
Alisema kuwa kituo hicho ambacho kinatoa huduma kwa wakazi wa kata tatu za Mwika kaskazini,Mwika Kusini na Mamba kwa siku za karibuni kimekuwa kikipata msongamano wa maiti nyingi kutoka Katika hosipitali jirani hivyo kukosa namna ya kuhifadhi kutokana na kukosa umeme wa uhakika ambao hutumika katika chumba chakuhifadhia maiti.
"Kwani siku za karibuni tumekuwa tukipata maiti nyingi kutoka hosipitali za karibuni ambazo zimezieiwa ila changamoto kubwa hapa hatuna nishati mbadala yaani umeme ukikatika basi tunaanza kuhaha ila ingekuwepo mbadala tungefanya kazi kea ufanisi zaidi tunaomba utukumbuke katika hili"alisema
Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutawezesha chumba cha kuhifadhia maiti kutoa huduma za uhakika tofauti na ilivyo sasa ambapo umeme umekuwa ukikatika Mara kwa mara na hivyo kufanya uendeshaji wa chumba hicho kutofanyika kea ufanisi licha ya kuwa ndio tegemezi kwa wananchi walio wengi.
Diwani wa Mwika Kaskazini Samweli Shao alisema kituo hicho kimekuwa ni msaada kwa kata takriban tatu na hivyo ipo haja kwa serikali kuona umuhimu wake ili kukiboresha kwani ni miongoni mwa vituo vikongwe vya afya katika wilaya ya Moshi.
"Kina msaada mkubwa lakini kinaonekana Kama kusahaulika hivyo nadhani mheshimiwa mbunge ipo haja Sasa ufikishe kilio hiki sehemu husika kwani mazingira ya kituo hiki hayaendani na nchi yenye uchumi wa Kati"alisema
Kwa upande wake Mbunge wa Vunjo Dkt Charles Kimei alisema amelezimika kutoa msaada huo wa mashuka kwa vituo mbali mbali vya afya Katika Jimbo hilo lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini.
Alisema kuwa kituo hicho kwa sasa kinahitaji ukarabati ili kiweze kutoa huduma kwa ufanisi na kwa kufanya hivyo kutaenda kupunguza msongamano Katika hosipitali nyingine.
"Nimefika na nimejionea mwenyewe uchakavu wa kituo hiki naombeno nifikishe kilio hiki kea wizara yenye dhamana ili ikiwezekana kiweze kupewa kipaumbele kwani kinavyozidi kubaki ndivyo uchakavu unaongezeka"alisema
Alisema kuwa hospitali nyingi zinazozozunguka kata hizo ni za binafsi hivyo wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu na kuwa sasa ipo haha kwa serikali kutambua umuhimu wa kituo hicho kwa kukikarabati ili kuweza kukiongezea uwezo.

0 Comments:
Post a Comment