MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KESI YA SABAYA



 KESHO mahakama ya hakimu mkazi Arusha  inatarajia kutoa uamuzi endapo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wana kesi ya kujibu au la.



Katika kesi hiyo inayofuatiliwa na wengi, Sabaya na wenzake  Silivester Nyengu na Daniel Mbura wanakabiliwa na mashitaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo amesema kuwa atatoa uamuzi huo Agosti 12, mwaka huu wakati wakati akiahirisha shauri hilo la jinai namba 105/2021 baada ya upande wa jamhuri kufunga  ushahidi wake.

Awali wakili wa serikali mkuu, Tumaini Kweka aliieleza mahakama hiyo kuwa wamefunga ushahidi baada ya kuwaleta mahakamani hapo mashahidi 11.

"Kupitia ushahidi wa shahidi wa 11,  ndiyo unahitimisha ushahidi upande wa mashitaka. Tunaiomba mahakama tufunge kesi yetu na kuiacha mahakama kuangalia ushahidi huo kuona ni nini kitafuata kwa mujibu wa sheria," wakili wa serikali mkuu Kweka ameeleza.

Alindelea kusema kuwa hawatawasilisha hoja za majumuisho kwani wanaiachia mahakama yenyewe kuamua lakini akaongeza kuwa endapo upande wa utetezi watawasilisha hoja za majumuosho na wao watazijibi.


Akiongea kwa niaba ya mawakili wa utetezi, Wakili Dancan Oola aliieleza mahaka hiyo kuwa hawana nia ya kuwasilisha hoja za majumuisho na wanaiachia mahakama kuamua kama washitakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Shauri hilo limesikilizwa mfululizo kuanzia Julai 19, mwaka huu ambapo upande wa jamhuri uliwaleta mashahidi 11 na vielelezo nane

Mashahidi hao ni pamoja na mmiliki wa duka la Shaahid Store, Mohamed Saad Hajirini ambapo washitakiwa wanadaiwa kulivamia februari 9 mwaka huu na kuwapekuwa kisha kuwaweka chini ya ulinzi wahudumu na wateja kisha kuwapiga vibao, mateke na ngumu huku wakiwatisha kwa silaha ili waonyeshe mmiliki huyo alipo.

Shahidi wa pili ni mtoto, Numan Jasin, (17) ambaye ndiye aliachiwa duka na mjomba wake kulisimamia ambapo aliieleza mahakama kuwa Sabaya alikuwa akiwaambia wasaidizi wake kuwatoa wenge watu walioingia dukani hapo kwa kuwapiga makofi kwenye masikio kisha kuwasachi na kuwaamuru kukaa chini.

Numan alieleza mahakamani hapo kuwa siku siku ya tukio Sabaya alimwamrisha ampigie mjomba wake simu ili afike hapo dukani na iliposhindikana ndipo akawaweka chini ya ulinzi ambapo walipekua na ku hukua mashine mbili za RFD  na fedha taslim 2,769,000.

Shahidi wa tatu mmachinga, Ramadhan Ayoub Rashid maarufu kama Anas (26)  ambaye aliieleza mahakama kuwa siku ya tukio  baada ya kuingia dukani hapo alipekuliwa na wasaidizi wa Sabaya wakachukua simu yake na fedha zake shilingi 35,000.

Shahidi wa nne ni Hajirini Saad Hajirini ambaye ni ndugu wa mmiliki wa duka hilo ambaye aliieleza mahakama namna Sabaya alipombana ikimtaka amuite Mohamed dukani hapo kisha akashushiwa kipigo.

Shahidi wa tano Seleman Kassim Msuya, (36), mfanyabiashara jirani na suka la Shaahid Store ambaye aliieleza mahakama namna alivyomuona Sabaya soku ya tukio akiwasili na msafara wa magari matatu akiwa na wasaiadizi wake wakasalimia kidha akaingia kwenye dula la Mohamed huku mlangoni kukiwa na vijana wawili wenye bastola.

Shahidi wa sita ni Bakari Msangi, (38) ambaye pia ni diwani wa kata ya Sombetini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) ambaye yeye alitumia siku sita kutoa ushahidi wake mahakamani hapo akieleza namna alivyopigwa, alivyotekwa na Sabaya na wasaidizi wake kisha  kuibiwa fedha zake shilingi 390,000 huku wakimtishia kwa bastola.

Shahidi wa saba ni Mkuu wa upelelezi wilayani Arusha, Gwakisa Minga ambaye aliieleza mahakama namna Sabaya alivyowapeleka Numan na Hajirini kituo cha polisi ili awafungulie mashitaka yanuhujumu uchumi pamoja na namna alivyompokea diwani Msangi akiwa na majeraha kisha akaelekeza achuliwe maelezo akaoelekwa hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.

Shahidi wa nane ni mke wa Msangi, Magdalena Mallya, (22) ambaye aliieleza mahakama namna Sabaya alivyomuelekezea silaha kichwani na mdomoni wakati alipokuwa akimuomba amsamehe mume wake kama amemkosea na amuache kwani yeye ni mgonjwa  na mtoto wao.

Shahidi wa tisa ni Inspekta, Evarist Mwamwngo ambaye aliieleza mahakama namna alivyosimamia gwaride la utambulisho ambapo shahidi Bakari Msangi aliweza kumtambua mshitakiwa wa tatu kwenye kesi hiyo, Daniel.

Shahidi wa 10 ni Dkt. Ngiana Mtui, (28) ambaye ndiye alimpokea na kumpatia huduma ya kwanza na matibabu anayedaiwa kuwa mhanga wa tukio la uvamizi, Bakati Msangi alipofika kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru ambapo aliwasilisha mahakamani hapo fomu ya polisi ya matibabu PF 3 aliyojaziwa mgonjwa huyo kama kielelezo.

Shahidi wa 11 ni Kachero wa polisi, DC, James, (31)  ambaye alikuwwa mpelelezi wa kesi hiyo ambapo pia aliwasilisha mahakamani hapo vielelezo ikiwemo leseni na namba ya mlipa kodi, (TIN) ya mmiliko wa duka la Saad Store Mohamed Saad Hajirini.

Pia aliwasilisha picha zinazoonyesha maeneo anayodaiwa kuumia shahidi wa sita Bakari Msangi ambapo aliieleza mahaka kuwa walipoenda kukagua eneo la tukio walikuta pembeni ya kaunta ya duka hilo kukiwa na maji na matone ya damu ambapo Numan alimwambia yale maji ni mmoja wa wafanyakazi wao alijikojolea akiwa chininya ulinzi wa Sabaya na wasaidizi wake.

Pia aliwasilisha mahakamani hapo  barua ya mkuu wa upelelezi wilaya ya arusha OC CIC kwenda kwa kamisheni ya uchunguzi kwa ajili ya kuzichunguza picha  mnato tano na barua ya majibu yenye muhuri wa taasisi hiyo.

0 Comments:

Post a Comment