WATATU WAFARIKI MACHIMBONI ARUSHA

 



WATU watatu wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kudondokewa na kufunukwa na kifusi kwenye machimbo ya moram.

Tukio hilo limetokea leo, Mei 3, 2021 majira ya saa 3 asubuhi kwenye machimbo yaliyo kwenye kijiji cha Engorora kata ya Kisongo.

Waliojeruhiwa ni pamoja na Msukuma mkazi wa Unga Limited,  Everest na Haruna Mbasa wakazi wa Ngorobob Mateves ambapo wanapatiwa matibabu kwenye zahanati ya Kisongo.

Waliofariki dunia ni Nurdin Rajab, Idd Huseni na Bonkila Martini, (26) wote wakazi wa Ngorbob Mateves.

 "Juhudi za uokoaji zimefanywa na wananchi na kutokana na tukio hilo, Wananchi watatu wamefariki na wananchi watatu wamejeruhiwa ambao tayari wamefikishwa zahanati ya Kidongo kwa ajili ya matibabu,"


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amewataka wataalam waende kufanyia uhakiki usalama wa migodi yote mkoani hapa

Amesema hataufunga mgodi huo isipokuwa wachimbaji wachukue tahadhari wakati wakiendelea na shughuli zao.
 


0 Comments:

Post a Comment