Paroko wa kanisa Katoliki, Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria Unga Limited, Padre, Festus Mwangwangwi |
WANAWAKE wametakiwa kuwaandaa watoto wao kwa ajili ya kuwa wanafamia bora wanapoingia kwenye maidha ya ndoa kwa kuwafanya kuwa wanaojielewa, wawajibikaji na wenye hofu ya Mungu.
Aidha wazazi wote, baba na mama wametakiwa kuishi maisha ya mfano kwa watotonna jamii inayowazunguka kwani watoto huiga toka kwa wazazi.
Hayo yameelezwa leo na Paroko wa kanisa Katoliki, Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited, Padre, Festus Mangangwi wakati akiongea na Wanawaka Wakatoliki wa jimbo kuu Katoliki kanisani hapo.
Akitoa mada juu ya nafasi ya mwanamke kuandaa wanandoa kwa watoto wao wa kike na wakiume, alisema kuwa jambo la kwanza wazazi wanapaswa wapandikize hofu ya Mungu kwa watoto wao ili wajue wakitaka kufanikiwa wahakikishe wanamtanguliza Mungu katika hatua zote za maisha yao.
Kauli mbiu ya jimbo Muondoko Kujitambua kuwajibika na kushirikiana katika Kristu.
"Wanandoa lazima wajitambue, umeshafunga ndoa mambo yale ambayo si mazuri uliyokuwa unayafanya kabla haujaingia kwenye ndoa usiyafanye tena na yale mazuri yawe mara mbili," amesema Padre Mangwanwi na kuongeza.
"Haipendezi kijana wa kiume umefunga ndoa kisha unalewa unachelewa kurudi nyumbani. Unakuta saa sita au saba usiku (wanawake wakapaza sauti "wanalala hukohuko") vitu kama hivi kwa wanandoa vinaleta ukakasi,".
"Kama vinakutokea na tayari wewe ni mwanandoa utakuwaje chachu ya kuwafanya wengine * kwenye ndoa waishi maisha hayo vizuri?".
"Chungeni ndoa zenu, heshimianeni, timizeni majukumu yenu kama wanandoa kadiri mnavyoishi kila siku ndivyo mnavyoandaa watoto wenu kwa maisha ya ndoa kesho,".
"Haipendezi binti anarudi likizo kutoka shule anapokuwa nyumbani hafui, hadeki, hapiki kisa eti emechoka kesho anaolewa huyu binti hajui hata kupika ndiyo wale wanawapigia simu waume zao wanunue chakula kutoka supermarket,".
Padre Mangwangwi amesema vitu hivyo huchangia ndoa nyingi kuingia dosari ambapo aliwahimiza wanawake hao kuzungatia usafi binafsi, wa nyumba wa mume zao pamoja na watoto kwa kile alichoeleza kuwa vitu hivyo vidogovidogo vinawachosha wanaume.
MSICHEPUKE YALE MNAYOYAFANYA KWA MICHEPUKO MYAFANYE NDANI YA NDOA
Aliwaeleza wanawake hao kuwa aliwahi kuhudhuria semina ya wanandoa nchini Uganda kwa miezi tisa ambapo wanandoa walikuwa wanaeleza uzoefu wa yale wanayoyapitia kwenye mahusiano ambapo ilionekana wanandoa wanakuwa hawana kitu cha tofauti jambo linalofanya yaibuke malalamiko miongoni mwao.
" Tunapata kesi nyingine unakuta mwanaume analalamika kuwa mke wake wanapokuwa pamoja haoni kitu cha ziada. Mwanaume analalamika "Sioni kitu cha ziada. Staili ndiyo ileile miaka nenda miaka rudi". Kwa hiyo mwanaume anatarajia aone cha ziada kwa mke wake wanapokuwa faragha," anasema Padri Mangwangi na kuongeza.
"Mambo hayo zamani yalikuwa hayasemwi lakini utandawazi huu yanasemwa, yule mama kule Uganda alikuwa anasema mke wa ndoa akichepuka anafanya cha ziada na ndiyo sababu mabuzi huwang'ang'ania,".
"Kama kuna mtu anatabia ya kuchepuka aache hakikisheni yale mnayofanya kwa michepuko mnayafanya kwa waume zenu ili naye asichepuke kwa jinsi hiyo ndoa zitadumu,".
HATARI YA MAPENZI YA JINSIA MOJA KWA WATOTO
Padre Mangwangwi amewataka wazazi wawaonye watoto hasa wale wanaosoma kwenye shule za wasichana au wavulana peke yao.
"Unakuta wengine walishaharibiwa nyumbani na baba. Unakuta baba kamharibu kijana wake wa kiume, sasa kijana anapoenda shuleni pengine yeye ndo alikuwa anafanyiwa vitendo vya ushoga anawalazimisha vijana wenzake wamfanyie hivyo unakuta vijana wengine wanaiga nao wanakuwa na tabia za ushoga," ameonya Padre Mangwangwi na kuongeza.
"Kijana anafikia umri wa kuoa wakiwa faragha anamtaka mke wake ageuke, ni kwasababu ameshazoea vitendo hivyo. Unakuta wengine ndiyo anafanyiwa hivyo ili aweze kushiriki tendo la ndoa na mke wake lazima ashogewe," anasema Padre huyo ma kuongeza.
"Vitendo hivi vya ushoga vinadhalilisha, vinahatarisha ndoa na vinakudhalilisha binafsi. Siku hizi tunaongelea ushoga na usagaji japo sasa wameanza kushiriki na wanyama,".
Amesema ukisoma kitabu cha Walawi Sura ya 8:1-25 Mungu ameongelea laana mbalimbali ikiwemo ya ndugu kwa ndugu kutenda matendo kama hayo.
"Imeandikwa na asionekane kwenu anayesimama mbele ya mnyama. Maana yake ukisimama mbele ya mnyama wewe ni mwanamke. Na asionekane kwenu anayesimama nyuma ya mnyama, maana yake nini huyu ni mwanaume. Kwa hiyo leo tusipokemea ushoga siyo tu kesho zitakuwa ndoa za ushoga bali zitakuwa ndoa za mbwa na wanadamu," alionya Padre Mangwamngwi.
UTANDAWAZI UNACHANGIA KUPOROMOKA MAADILI -MANGA
Mwenyekiti wa Wanawake Wakatoliki Tanzania, (WAWATA) Jimbo Kuu Arusha, Bakhita Manga amesema kuwa mafunzo waliyopewa na Padre Mangwangwi ni yenyr manufaa kwani yamesisitiza umuhimu wa wao kama wanawake kusimama kwenye nafasi zao katika kuwaanda watoto wao kuwa wake na waume wema.
"Pamoja na upendo lakini kuna mambo mengine ya kuangalia. Ndoa inaongozwa na upendo lakini hasa imani na sala ndiyo itasababisha hiyo ndoa iweze kudumu," amesema Manga ambaye pia ni mwenyekiti wa WAWATA Kanda inayojumuisha jimbo la Moshi Same, Mbulu na Arusha
Suala la wanawake kuwaachia majukumu mengi wasichana wa kazi amesema,"Unajua kwa sasa dunia imebadilika na utandawazi ni mkubwa zaidi. Maadili ya sasa na zamani ni tofauti kidogo kwa sasa kuna mporomoko mkubwa wa maadili. Ndiyo sababu baba Paroko ameweka msisitizo hapo,".
"Zamani mpaka inafikia mwanamke au mwanaume kuoa au kuolewa lazima hata wazazi huwa wanachangia anaweza kushauri usiende nyumba fulani si kwamba walikuwa hawapendi ila kikubwa sana wao walikuwa wanafuata maadili,".
Manga amesema kuwa kwenye suala la ndoa kusambaratika huweza husababishwa na mwanamke au mwanaume kama ambayo kwenye semina baba Paroko ameeleza mwanaume mwanaume anaweza kutoka anaenda kukaa mahali zaidi bila ya kuwa na familia yake naye mwanamke akitoka kwenye majukumu yake ya kazi akifika nyumbani anakaa bila kujishughulisha.
"Hivyo wote wawili wanaweza kuwa chanzo kutokana na kutojitambua katika wajibu wao wa ndoa. Hivyo kikubwa wanandoa tufuate imani, tuzingatie maadili na tunapoingia kwenye ndoa tuingie kikamilifu sio roborobo. Sakramenti ya ndoa si ya kuichezea ni sakramenti ya kuitumikia ipasavyo," amesisitiza Manga.
Wanawake wa jimbo hilo hukutana kila jumapili ya pili ya mwezi kwa ajili ya Kusemezana ambapo huwawezesha kuinjilishana kupitia mada mbalimbali zinazowajenga kiroho, kimwili na maswala ya kiuchumi
0 Comments:
Post a Comment