Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) amesema Demokrasia ni pamoja na kuheshimu Taasisi zinazounda Demokrasia ikiwemo Vyama vya Siasa.
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amehoji sababu ya Bunge kuendelea kuwatambua wabunge 19 wa viti maalum waliofukuzwa Chadema na kutaka uamuzi wa chama hicho kuheshimiwa.
Wabunge wa hao wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee walifukuzwa kwenye chama hicho Novemba 27, 2021 baada ya kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa bila idhini ya Chadema.
“Sasa hivi kuna Wanachama wapo Bungeni wa CHADEMA lakini CHADEMA ilishawafukuza. Kwanini wapo Bungeni? Wanatakiwa wasiwepo. Tufuate Sheria”, amesema Nape
Amesema Mfumo wa Vyama vingi ulipokuja Katiba ilibadilishwa na Tume mbalimbali zilipendekeza namna ya kuendesha Vyama vingi ikiwemo Tume ya Jaji Nyalali.
“Tumepitia Milima na mabonde kwenye Siasa hadi hapa tulipofikia. Wapo walioumia na Wengine kufurahi. Rais Samia katoa Uwanja wa Meza ya Mzungumzo. Kwakuwa yupo tayari kukaa meza moja, basi tusikatae mazungumzo”, amesema Nape.
Hata hivyo, walikata rufaa Baraza Kuu la Chadema kupinga kufukuzwa lakini mpaka leo hawajasikilizwa.
Mbali na Mdee, wengine waliofukuzwa Chadema ni Ester Bulaya, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Hawa Mwaifunga, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Salome Makamba na Jesca Kishoa.
Wengine ni Tunza Malapo, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Conchesta Rwamlaza, Cecilia Pareso, Agnesta Lambert, Asia Mohammed, Stella Fiao na Felister Njau.
Akizungumza jana Ijumaa Aprili 23, 2021 katika mdahalo uliowahusisha viongozi wa vyama vya siasa ulioendeshwa kupitia mtandao wa Zoom kupitia ukurasa wa Nadj Media Center, Nape amesema suala hilo liko wazi kwamba hawastahili kuwa wabunge kwa mujibu wa katiba.
0 Comments:
Post a Comment