KADA wa chama Cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Moshi Vijijini Emanuel Mlaki amewataka vijana kutumia fursa zilizopo kwa kujiajiri sambamba na kuzalisha ajira kwa ustawi wa taifa badala ya kusubiria ajira.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi Mchango wake wa mifuko kumi (10) saruji kwa uongozi wa Chama na UVCCM wilaya ya Hai ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake katika kuunga mkono alengo ya UVCCM taifa ya Ujenzi wa Nyumba za Watendaji wa jumuiya ya vijana katika wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro.
Amesema vijana hawana budi kushiriki kwa vitendo kwa kujishughulisha na miradi mbalimbali ya kimaendeleo badala ya kusubiria kuajiriwa na kuwa shughuli watakazokuwa wanazifanya zina uwezo wa kuzalisha ajira na kupunguza ombwe la ajira hususan kwa vijana
Tukio hilo pia limehudhuriwa na Katibu wa CCM Wilaya Ndg. Kumotola,Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya Ndg. Innocent Mallya,Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Ndg.Imrani Shoo,Katibu wa UVCCM Wilaya Ndg.Julius Msaka,Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya Khayrath Nkinga na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya Ndg. Lilian Kimario & Emanuel Bujiku.
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Hai Kumotola Kumotola amesema vijana wengi wana maono ila tatizo kunwa wamekuwa wakikatishwa tamaa Jambo ambalo sio jema kwa afya ya taifa kwa siku zijazo
Henrry Munisi mkazi wa Bomang'ombe amesema vijana walio wengi hawajaandaliwa kujiajiri Jambo ambalo ni tatizo kubwa na kuwa ipo haja ya Sasa kwa vijana kujitafakari upya.
.
0 Comments:
Post a Comment