Nimeona jinsi mlivyommwagia sifa Bungeni na baadae mkamuunga mkono kwa asilimia 100. Mhe. Dkt. Mpango hongera sana kwa kutwikwa madaraka mengine katika ngazi hii. Nilizunguka sana kutafuta, nikaangalia ndani ya Bunge na nje ya Bunge lakini nikarudi ndani ya Bunge – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mtu niliyemuona anafaa kwa sasa hivi ni ndugu Philip Isdor Mpango. Philip ni mcha Mungu, Philip ni mchumi mahiri, mchapakazi na hodari – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mbali na majukumu yake yaliyowekwa kikatiba, Dkt. Mpango atakwenda kunisaidia kwenye mambo ya kiuchumi na kwenye udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali, nimeona ndio mtu sahihi wa kwenda nae katika majukumu yetu haya – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Kuondoka kwa Dkt. Mpango katika Wizara ya Fedha na Mipango kumueacha nafasi ndani ya Wizara hiyo na tupo kwenye Bunge la Bajeti ambalo Waziri wa fedha ni muhimu sana kuwepo - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Nimeona nisifanye kazi kidogo kidogo na nimelitazama upya Baraza la Mawaziri na kufanya mabadiliko madogo katika Baraza hilo. Zege hailali, ni hapahapa nitalitaja - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Nimemteua Balozi Hussein Yahya Katanga ambaye ni Balozi wa Tanzania, nchini Japan kuchukua nafasi ya Bashiru Ally aliyekua Katibu Mkuu Kiongozi - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Niwaombe sana mkafanye kazi zenu, kila mmoja katika Wizara yake, kila mmoja katika pahala pake, akafanye kazi. Manaibu Mawaziri wakatumike vizuri, kuna mtindo wa kutokuwapangia kazi na kudharauliana. Hata sasa nina kesi za Manaibu Mawaziri kudharau Mawaziri na Mawaziri kudharau Manaibu wao. Hii tabia siitaki, ninachotaka ni kazi na sitaki kusikia kingine - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Sikuwahi kuota wala kutarajia mimi mtoto wa masikini kutoka kwetu Buhigwe, ningepata nafasi ya kutumikia taifa letu katika nafasi hii ya Makamu wa Rais. Nakuahidi nitakuwa msaidizi muaminifu, mtiifu na mzalendo kwa nchi yangu – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango
Nitatekeleza kwa bidii na weledi kazi zote utakazoniagiza pamoja na majukumu mengine kama yalivyoelekezwa kwenye Katiba kwenye ile Ibara ya 47. Nitatekeleza majukumu hayo chini ya uongozi na usimamizi wako, nipo tayari kuchapa kazi, nitume mchana na usiku - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango
Nitashirikiana na viongozi wenzangu, pande zote za Muungano lakini pia mihimili yote ya Dola. Nawashukuru Watanzania wote kwa kudumisha amani na umoja wakati wote - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango
______________________
Mhe. Mpango namfahamu vizuri, nimefanya naye kazi, yeye akiwa Waziri wa Fedha na mimi nikiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Mhe. Mpango ni mtu mwenye weledi mkubwa, mchapakazi na muadilifu sana – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi
Tunakuombea kwa Mungu akusaidie katika majukumu yako mapya na sisi tutakupa ushirikiano wote utakaohitaji - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi
Sheria huwa haina tatizo lolote lakini sheria ikitumika vibaya huwa inakuwa hatari sana kwa maendeleo ya nchi.
_________________________
Nawaomba tufanye kazi zetu, tusipeleke vitu vidogovidogo kwa Mhe. Rais na Mheshimiwa Makamu wa Rais. Tuwaache wafanye kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu – Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma
_________________________
Kwa upande wake, Spika wa bunge, Job Ndugai, alisema Makamu wa Rais, Philip Mpango alipata kura ambazo huwa ni nadra sana kuzipata.
" Alipata kura za Wabunge wote. Tunakutakia kila la kheri Mhe. Mpango, tunakuaminia na tunaamini utamsaidia Mhe. Rais katika kazi zake," alisema Ndugai na kuongeza
Bunge la Bajeti limeanza kazi yake. Kazi hii ni kubwa, nzito na inahitaji majadiliano. Kazi hii inahitaji sana Waziri wa Fedha na Mipango, hii itatusaidia kupanga vizuri pale Bungeni – Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai
0 Comments:
Post a Comment