WAFANYABIASHARA jijini Arusha waonyesha matumaini makubwa na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Wakiongea na waandishi wa habari wafanyabiashara hizo leo Machi 19, mwaka huu walisema wamepitia historia ya mama Samia kwenye uongozi wameona ni mtu makini, mwenye uzoefu wa kutosha kuongoza nchi isonge mbele.
Mfanyabiashara maarufu, Philemon Mollel maarufu kama Monaban alisema kuwa anaamini mipango na miradi mingi ya awamu ya tano itaendelea kwani Rais Samia alikuwa ni Makamu wa Rais hivyo anaijua vema.
"Nimpe hongera sana Rais, Samia Suluhu Hassan kuapishwa kuwa Rais, sina wasiwasi na mama Samia kwa sababu ni kiongozi mwadilifu ni kiongozi ambaye kwa kweli tunamtegemea," anasema Monaban na kuongeza.
...Nitoe pole kwa Watanzania wenzangu, maswali yako mengi. Watu wengi ninaokutana nao na zaidi wanachojiuliza je kile kichoanzishwa na hayati Rais Magufuli kitaendelea?....
... Wanauliza miradi mikubwa itaendelea na huu ndiyo mtihani mkubwa wa CCM na serikali yake. Kwamba vile vilivyoanzishwa viweze kuendelea ili kutimiza matamanio ya Watanzania yaweze kufika mahali thabiti....
.....Kwa sababu ni ukweli Rais wetu (Hayati Magufuli) alituonyesha dira, alituonyesha mahali tulipokuwa, tulipo na tunapokwenda taarifa ya kifo chake imekuwa kama mshale imetuchoma mioyoni mwetu .....
Monaban alisema kuwa anawaomba viongozi CCM na Serikali kuvaa viatu vya hayati, Magufuli ili waongoze kufikia malengo ambayo kama Taifa tulikusudia kuyafikia ya kutoka uchumi wa kati kwenda uchumi wa juu.
"Nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wetu, Samia Suluhu Hassan ambaye leo ameapa kuliongoza Taifa letu, ninamuombea kwa Mungu ya kwamba ataweza na amtegemee Mungu," alisema Monaban na kuongeza .
...Kwa sababu kama Hayati, Rais Magufuli alikuwa anasema kifo kipo. Maandiko yanasema maisha ya mwanadamu ni miaka 70 ukiwa na nguvu ni miaka 80. Hivyo hakuna haja ya kuogopa kwani kifo kipo tuishi kwa unyenyekevu tukipendana...
...Niwaombe Watanzania msiba unapotokea, watu huzika tofauti zao za huko nyuma. Niwaombe Watanzania msiba huu utulete pamoja bila kujali tofauti zetu za kidini, kikatiba na kiitadi.....
Mkurugenzi Mtendaji wa Benson & Company LTD, Naushad Mohamedhussein alisema kuwa tokea Rais, Samia alitangazie Taifa Msiba wa Hayati, Magufuli na yeye kuapishwa kuwa Rais ameendelea kuwa nguzo kwa wananchi kwa kuwapa faraja.
"Rais Samia ana hekima na busara, ni mama mpole msikivu anaongez kwa upole lakini anamaanisha. Akisema nataka kazi zangu zifanyike vizuri ukimuangalia usoni unaiona hekima," anasema Naushad na kuongeza.
"Tunamtakia kila la heri, mimi ni mtu wa Zanzibar, uzoefu wangu watu wa Zanzibar wanakuwa ni wapoole sana, tunamtakia kila la kheri,".
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda cha vinywaji cha Raha, Adolf Olomi alisema kuwa watamkumbuka Rais Magufuli kwa kupigia debe na kuvipigania viwanda kwa vitendo ambapo alikubali kuwa mlezi wa taasisi ya wenye viwanda nchini.
Katika kipindi chake ameanzisha mifumo mingi ya uendelezaji wa viwanda. Mfano mzuri ni wa 'electronic stamp' katika biashara za vinywaji kama za kwetu kuna maeneo mengi kuna udanganyifu katika uzalishaji lakini pia kangiza bidhaa kutoka nje bila kulipia kodi hivyo utumiaji wa electronic stamp umekuwa ni dawa kwa wale wadanganyifu kwani kwa sasa wote wanalipia kodi.
Alisema ameweza kuboresha mifumo ya utendaji wa watumishi wa umma ambapo kwa sasa watu wamekuwa wakifanya kazi kitaalamu na kwa ufanisi zaidi hata ukiandika barua unajibiwa kwa wakati tofauti na miaka ya nyuma ambapo huduma kwenye ofisi za umma ilikuwa si nzuri sana.
Tumepata Rais Samia Suluhu Hassan ni mama makini tunamuamini, kwa sababu mifumo iliyowekwa na Hayati, Rais, Magufuli ataenda kukanyaga kule walipokuwa wakikanyaga wakiwa wanaongoza," alisema Olomi na kuongeza.
"Hapa alipoanzia mama Samia amekuta msingi mzuri, na mimi nina imani kubwa naye kwani hafanyi kazi peke yake anafanya kazi na timu ya viongozi makini walichujwa na hayati Magufuli wakawekwa kwenye mamlaka hivyo tunaamini tunaenda kufanikiwa,".
0 Comments:
Post a Comment