UMOJA WA VYAMA VYA SIASA ARUSHA WAMLILIA JPM

 


UMOJA wa vyama vya siasa Mkoa wa Arusha umetoa pole kwa familia ya Hayati Rais John Magufuli kwa kumpoteza Rais ,familia sanjari na watanzania kwa ujumla.


Salamu hizo za pole zimetolewa Machi 19, mwaka huu na viongozi wa vyama vya upinzani tofauti Jijini Arusha,ambapo kwa pamoja wamemuomba Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan, kusimamia yale yote mazuri yaliachwa na Hayati, Rais Magufuli ili kumuenzi na kuipeleka nchi ya Tanzania katika uchumi wa kati na kuinua fursa za viwanda .

" Lala salama Hayati  Rais John Magufuli  kwani ulikuwa ni kiboko ya mabepari,mpigania haki za wanyonge hasa machinga tunakuombea kwa mola mungu apumzishe roho yako mahala pepa peponi," alisema Naibu Katibu wa chama cha Demokrasia Makini Mkoa wa Arusha,Simon Ngilisho 

Alisema, hayati Rais Magufuli amefanya mengi katika uongozi wake hivyo yale aliyoyaacha yaendelezwe kwa usimamizi wa Rais Samia Hassan Suluhu kwani ni mama shujaa,anayejua wananchi wanahitaji nini na kamwe watumishi waliopo madarakani wasidhani kuwa wanawake hawawezi bali wanawake wanaweza kuleta maendeleo katika kuhakikisha ngazi za familia zinakuwa bora sanjari na kumudu majukumu mengine ya kiungozi.


"Tutampa ushirikiano wa kutosha mama Samia na tunamuombea Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa mola ampe nguvu zaidi katika kipindi hiki," alisema Ngilisho.



Kwa upande wake,  Mwenezi wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Mkoa wa Arusha, Geofrey Stephen alisema TLP itamuunga mkono Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan kwani awali chama hicho kinaimani kubwa na serikali na kinatoa pole kwa msiba huu uliotokea wa kifo cha Rais Magufuli.


"Hayati Rais, Magufuli amefanya mengi na ameacha mengine yanayostahili kuendelezwa hivyo ni vema yakaendelezwa kwani serikali ipo dhabiti tuenzi uzalendo wetu na kuhakikisha Taifa letu linakuwa na umoja na kushikana mikono ili Taifa lisonge mbele," alisema Steven.


Wakati huo huo,Mwenyekiti wa Sauti ya Umma, (SAU) Mkoani Arusha, Simon Bayo alisema wamempoteza kiongozi  shujaa Afrika mwenye udhubutu katika maamuzi magumu na alitoa pole nyingi kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan , watanzania, viongozi mbalimbali wa dini,serikali na kusisitiza zaidi amani,mshikamano udumu zaidi katika kuhakikisha serikali 


Wakati huo ,Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini Tanzania, Sammy Mollel amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha hayati Rais John Magufuli kwani alikuwa jemedari katika kusimamia biashara  ya madini


Mollel aliyasema hayo jana wakati akizungumzia kuhusu msiba wa Rais John Magufuli na kuongeza kuwa Rais Magufuli alisimama kidete katika kuhakikisha sekta ya madini inaleta tija kwa wananchi,nchi ikiwemo kuleta heshima ya nchi kwa kudhibiti utoroshaji wa Madini.



0 Comments:

Post a Comment