Kuondoka kwa Dkt. John Pombe Magufuli kumetikisa bara la Afrika. Bara la Afrika "linajikuta hayati" kwa kupoteza mwanasiasa mkongwe na kiongozi aliyelenga kuboresha maisha na kulinda maslahi ya wananchi wake - Félix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Tutabaki na kumbukumbu ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kama Mpiganaji na Mzalendo. Sio tu kwa watu wa Tanzania bali kwa Afrika nzima, mtetezi mkuu wa Uhuru wa kiutamaduni na kiuchumi wa bara la Afrika - Félix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Sisi kama Wakenya na mimi binafsi, tulisema lazima tuje kumsindikiza ndugu yetu. Tutaendelea kufanya kazi pamoja na kushirikiana na hatimaye kuleta Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bara la Afrika Pamoja – Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Tumeona kazi ya barabara, tumeona kazi ya umeme, tumeona kazi ya ujenzi wa viwanja vya ndege na miradi mingine mingi ambayo itaenda kuleta manufaa kwa Watanzania na manufaa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukuza biashara. – Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Niko hapa kumuomboleza rafiki wa karibu, mtu ambaye tuliongea mara kwa mara tukibadilishana mawazo kuhusu nchi zetu na Jumuiya ya Afrika Mashariki - Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Leo Afrika imepoteza mtu mashuhuri, leo wananchi wa Tanzania wamempoteza raia muaminifu, mfanyakazi na mwenye Imani ya kipekee iliyokuza taifa la Tanzania na bara la Afrika - Mhe. Felipe Nyusi, Rais wa Msumbiji
Utulivu wa kisiasa wenye sifa nzuri na za wazi, ustawi wa kijamii na kiuchumi wa Tanzania, miundombinu ya msingi kwa ajili ya kuboresha hali ya maisha ya Watanzania, viwango vya juu vya ufanisi na utendaji bora wa Serikali ni matunda ya uongozi wa Rais Magufuli - Mhe. Felipe Nyusi, Rais wa Msumbiji
Umoja wa Familia ya Afrika leo unaomboleza kwa kuondokewa na kiongozi mahiri ambaye alikua na maono ya kulikomboa bara la Afrika. Tumempoteza mtetezi wa Afrika aliyesimama bila uoga kulitetea bara la Afrika - Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini
Bado nakumbuka Rais Magufuli alivyokuja Afrika Kusini wakati naapishwa na akanipa maono na dira aliyonayo kwa nchi ya Tanzania na watu wake. Nilifarijika sana kwasababu Rais Magufuli hakuwa mtu wa kusafiri sana, alipendelea kukaa nchini kwake - Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini
Serikali na wananchi wa Visiwa vya Comoro tunatuma salamu za rambirambi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Mama Samia. Kuondoka kwa Dkt. John Pombe Magufuli ni pigo kubwa sana kwa bara la Afrika, dunia na kwa Visiwa vya Comoro - Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani
Nchi ya Comoro ipo kwenye msiba mkubwa sababu Comoro na Tanzania ni kitu kimoja na vitu vinavyo tuunganisha ni vingi ikiwemo historia, jiographia, lugha na malengo yote yenye nia ya kuleta maendeleo kwa wananchi wetu. Bara la Afrika limepoteza mtu mkubwa sana aliyeweka bara hili mbele - Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani
Miezi kadhaa iliyopita, mimi na Rais Magufuli tulipata chakula cha jioni Ikulu Dar es salaam, sikufahamu kuwa ndio ingekua mara ya mwisho kukaa naye na kupata chakula cha jioni. Alinisindikiza mpaka kwenye uwanja wa ndege, lakini sikijua kama ndio ingekua mara ya mwisho kuonana - Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera
Waliosema wala rushwa na wanaokandamiza Serikali na nchi za Afrika hawawezi kukabiliwa hawakutegemea Magufuli angesimama kidete kupambana nao, waliosema nchi za Afrika haziwezi kuingia uchumi wa kati katika kipindi cha muhula mmoja wa uongozi hawakutegemea Magufuli angefanikisha hilo - Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera
Rais Magufuli alikuwa rafiki yangu wa karibu sana na nitamkumbuka sana. Maombi yetu tunatuma kwa familia na wananchi wote wa Tanzania. Tunaomba mwenyezi Mungu awapunguzie majonzi na kuwapa nguvu katika kipindi hichi kigumu – Rais wa Zambia, Edgar Lungu
Siku ya leo ni siku ya giza sana hapa Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla. Sisi watu wa Zimbabwe tuliumia sana sababu Rais Magufuli alijitoa kuitumikia Tanzania na Bara la Afrika - Emmerson Mnangagwa, Rais wa Zimbabwe
0 Comments:
Post a Comment