Mahojiano ya Oprah: Ufalme wa Uingereza umesema unafuatilia maoni ya meghana na mwanamfalme Harry dhidi ya ufalme huo kwa umuhimu mkubwa
Masuala ya ubaguzi wa rangi yaliyoibuliwa na Mwanamfalme Harry na mke wake katika mahojiano yao na Oprah Winfrey yanachukuliwa kwa "uzito mkubwa", Taarifa imetolewa kutoka makazi ya ufalme Buckingham.
Taarifa hiyo kutoka makazi ya mfalme imesema "huenda kumbukumbu zikatofautiana "lakini suala hilo litashughulikiwa kwa faragha.
Meghan alimwambia Oprah Harry aliulizwa na mtu wa familia ambaye hakutaka kumtaja mtoto atakayemzaa Archie, atakuwa "mweusi" kiasi gani.
Makazi ya Kifalme yamesema Mwanamfalme Harry na mke wake "watakuwa wanafamilia wanaopendwa".
Taarifa hiyo imetolewa na makazi ya Mfalme baada ya kufanyika kwa mikutano ya dharura iliyohusisha wanafamilia waandamizi wa Kifalme.
Familia ya Kifalme imekuwa chini ya shinikizo kubwa kujibu madai yaliyoibuliwa na Meghan - mtu wa kwanza kabisa katika familia ya Kifalme mwenye asili mchanganyiko kusema kwamba kulikuwa na maswali juu ya mtoto atakayemzaa.
Mwanamfalme Harry baadaye akaweka wazi kwa Oprah kwamba suala hilo halikuwa limeibuliwa na Malkia wala mume wake Duke wa Edinburgh.
Taarifa kutoka makazi ya Kifalme imetolewa siku moja unusu baada ya kufanyika kwa mahojiano yaliyopeperushwa hewani nchini Marekani na imesema: "Familia yote imeachwa na masikitiko makubwa baada ya kufahamu changamoto walizopitia Harry na Meghan miaka michache iliyopita.
"Masuala yaliyoibuliwa hasa la ubaguzi wa rangi linafuatiliwa kwa karibu. Huenda baadhi ya kumbukumbu zikatofautiana lakini yanachukuliwa kwa uzito mkubwa na yatashughuikiwa na familia kwa njia ya faragha.
"Harry, Meghan na Archie daima watakuwa wapendwa wa familia hii."
Pia inafahamika kwamba familia ya kifalme ilitaka kuangazia kwa kina jibu lao na kutoa fursa kwa raia wa Uingereza kutazama mahojiano hayo kwanza ambayo yalipeperushwa hewani Jumatatu usiku.
Inasemekana kwamba familia ya kifalme inachukulia suala hili kuwa la kifamilia na inaamini kwamba inastahili kupewa muda wa kulijadili kwa faragha.
Katika ziara yake London ambayo ilifanyika mapema, Mwanamfalme Charles hakujibu alipoulizwa ikiwa ameona mahojiano hayo ambapo Mwanamfalme Harry na mkewe waliangazia masuala binafsi ya ubaguzi wa rangi, afya ya akili, vyombo vya habari na watu wengine wa Familia ya Kifalme.
Jumatatu Uingereza ilipeperusha mahojiano hayo yaliyotazamwa na watu karibu milioni 11.1.
Katika mahojiano hayo, Meghan alisema kwamba kuna kipindi "hakutaka kuendelea kuishi" kwasababu alikuwa ameona familia ya kifalme ni ngumu sana. Alisema kwamba aliomba msaada kutoka Makazi ya Kifalme lakini hakupata.
Meghan alisema mazungumzo ya vile mtoto wake Archie atakavyokuwa mweusi huenda yalitokea wakati alipozaliwa na majadiliano juu ya kwanini hatapewa cheo cha kifalme na ulinzi wa polisi.
Chini ya sheria ambazo zimekuwepo tangu mwaka 1917, watoto wa wanandoa hao moja kwa moja hawatakuwa mwanamfalme na binti mfalme pengine Malkia aingilie kati.
Alipoulizwa na Oprah ikiwa kulikuwa na wasiwasi kuwa mtoto wake angekuwa "atakuwa mweupe sana" na hilo huenda likawa tatizo, Meghan alisema: "Ikiwa hiyo ndio dhana inayoiweka, basi hiyo ni salama zaidi."
Mwanamfalme Harry
Lakini wanandoa hao walikataa kusema ni nani hasa katika familia alisema maneno hayo. "Hayo, Siwezi kusema wazi," alisema mwanamfalme Harry. "Wakati huo ilikuwa vibaya, Ilishutua."
Harry pia alisema inauma kuona kwamba hakuna mtu hata mmoja wa familia ambaye aliwahi kuzungumza kumuunga mkono Meghan baada ya kugonga vichwa vya habari.
Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer amesema madai ya Meghan juu ya ubaguzi wa rangi na ukosefu wa uungwaji mkono katika afya ya akili yanastahili kuchukuliwa kwa "uzito mkubwa".
Inasemekana kwamba Waziri Mkuu Uingereza Boris Johnson alitazama mahojiano hayo Jumatatu usiku lakini akakataa kusema lolote


0 Comments:
Post a Comment