CHAMA cha wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya nchini, (TUGHE) mkoani Arusha imetoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu kwa wajane walio na uhitaji wenye watoto wategemezi zaidi ya wanne.
Wametoa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni moja Machi 6, mwaka huu jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mkoani Arusha mgeni rasmi akiwa, Kenan Mwangosi ambapo kilele huwa Machi 8, kila mwaka.
Mwenyekiti wa kamati za Wanawake wa TUGHE mkoani Arusha, Kabula Sukwa alisema kuwa alitafuta kaya ambazo zina uhitaji mkubwa sana wakazipata familia nane za wajane.
" Kwenye hizo familia nane na kila mmoja ana watoto zaidi ya watatu. Tulipofuatilia maisha yao tulibaini hawamudu kiziendesha familia zao kwani wana uhitaji mkubwa wa chakula," anasema Sukwa na kuongeza...
....Tukakaa kama kamati tukaamua tuwaandalie vyakula leo tumewakabidhi kila mmoja kilo 20 za mchele, kilo 10 za unga wa sembe, kilo 10 za maharage na lita tano za mafuta ya kupikia chakula pamoja na sabuni.


0 Comments:
Post a Comment