DIWANI ATAKA TANROADS KUWAONDOLEA KERO MACHINGA WA NJIA PANDA



IKIWA kesho March 8,ni  maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, wanawake  ambao ni wajasiriamali wadogowadogo katika eneo la mizani mpya kata ya Njiapanda wameiomba serikali kuona namna yakuwasaidia kufanya biashara zao bila bugudha tofauti na Sasa.


Mary Kamili ni mmoja wa wajasiriamali hao,  amesema licha ya serikali kuwapa vitambulisho vya wajasiriamali wadogowadogo vinavyowapa ruhusa ya kufanya shughuli zao bado wamekuwa wakizuiliwa kufanya hivyo katika eneo la mizani mpya iliyopo mamlaka ya mji mdogo wa Himo.


Alisema kuwa kumekuwepo na urasimu katika uendeshaji wa shughuli zao jambo ambalo linawakwamisha na kuwa vitambulisho walivyopewa na kuvilipia vinakuwa havina manufaa kwa upande wao.


"Tunateseka kwa kufukuzwa kama wakimbizi sasa tunashindwa kuelewa vitambulisho tulivyokata vinatusaidia nini hapa Njiapanda na timeaminishwa kuwa ni ruhusa kufanya kazi popote bila kuvunja sheria "alisema 


Alisema lengo la serikali iliyopo madarakani ni kuhakikisha kila mjasiriamali mdogo ananufaika na fursa kadri zinavyojitokeza lakini kwao jambo hilo limekuwa ni kinyume na kuwa mwisho wake hujulikani



Loveness Mfinanga ni diwani wa kata ya Njiapanda, alisema kilio cha wajasiriamali hao kimemfikia na kutaka mamlaka husika ikiwemo wakala wa barabara nchini (TANRODS) kuangalia njia sahihi yakuwasaidia kuliko ilivyokuwa sasa.


Alisema serikali ya awamu ya tano ilirasisimisha wajasiriamali kwa kuwapa vitambulisho hivyo kuzuiwa kwa wanawake hao kufanya shughuli zao ni sawa na kukiuka agizo ama maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli.


"Zitaenda kutumika njia rafiki hapa kwa sababu lengo si  kuwaondoa hawa wajasiriamali kwani ukiwekwa utaratibu mzuri mambo yatakuwa sawa kwani wameanza leo?mbona wapo siku zote?"alihoji.

Imendikwa na Gift Mongi, Moshi



0 Comments:

Post a Comment