![]() |
| Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Salum Hamduni akionyesha moja ya silaha aina ya gobore zinazopelekwa makao makuu ya polisi kwa ajili ya taratibu za kuteketezwa |
JUMLA ya silaha 126 zilizohusika na makosa dhidi ya wanyamapori kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia 2010 mpaka 2020 zimepelekwa makao makuu ya jeshi la polisi nchini kwa ajili ya kuharibiwa.
![]() |
Mkuu wa Kikosi Dhidi ya Ujangili, (KDU) Kanda ya kaskazini kilicho chini ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori, (TAWA), Mbanjoko Manyenga. |
![]() |
| Askari wa KDU wakipakia silaha hizo kwenye gari tayari kwa ajili ya kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi. |
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Salum Hamduni ameyasema hayo leo wakati akongea na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Mkuu wa Kikosi Dhidi ya Ujangili, (KDU) Kanda ya kaskazini kilicho chini ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori, (TAWA), Mbanjoko Manyenga.
Amesema kuwa katika silaha hizo 126, 125 ni magobole na moja ni Semi Automatic Rifle.
"Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa na silaha hizo kutaifishwa," alisema kamanda Hamduni na kuongeza
.... Baada ya taratibu zote kukamilika silaha zote zinatarajiwa kupelekwa makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya taratibu za kuharibiwa ili zisiweze kuingia tena kwenye shughuli za kiuhalifu ikiwa ni pamoja ya mitandao ya ujangili,".
Kamanda Hamduni alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa polisi, Kikosi Dhidi ya Ujangili na vyombo vingine vya usalama ili kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na ujangili.




0 Comments:
Post a Comment