MKURUGENZI HOTELI ZA NAURA SPRING ,IMPALA ACHARUKA MAHAKAMANI


Mkurugenzi wa hoteli za kitalii za Naura Spring na Impala, Pelagia Mrema leo akiwa kwenye viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha

Baadhi ya wafanyakazi wa hoteli za Naura Spring na Impala wakiwa kwenye viwanja vya mahakama kufuatilia kesi yao



MKURUGENZI wa Impala Hoteli za kitalii za Impala na Naura,  , Pelagia Mrema, amewakana mawakili wanaowakilisha hoteli hizo mahakama kuu kanda yaArusha kwa kile alichodai kuwa hawatambui.

Aidha alisema yeye na familia wameridhia mali za Impala  ziuzwe ili kulipa madeni ya hoteli hizo ikiwemo mishahara ya wafanyakazi huku akisisitiza apendezwi namna wafanyakazi hao wanavyohangaika kufuatilia mishahara yao.

Mkurugenzi huyo alisema hayo leo mbele ya jaji, Mohamed Gwae wa mahakama kuu kanda ya Arusha anayesikiliza maombi ya kuzuia mnada wa kuuza mali za hoteli hizo ili kufidia malimbikizo ya mishahara  ya wafanyakazi.

Mrema  alimweleza jaji kuwa yeye amefika mahakamani hapo kama mkurugenzi aliyebaki baada ya mkurugenzi mwenzake, Maleu Mrema kufariki na kuwa msimamo wake na familia mali hizo ziuzwe ili kulipa madeni.

" Mimi nimekuja kama mkurugenzi aliyebaki, siwatambui hawa (mawakili) walioleta shauri hili. Hata wasimamizi wa miradhi mali za marehemu (mkurugenzi mwenzake marehemu Maleu Mrema) wamepingwa mahakamani," alisema Mrema.

Hata hivyo jaji, Gwae alimkatisha akimwambia hoteli zake zinawakilishwa na mawakili mahakamani hapo ambapo Mrema akasema hawatambui jaji akamuuliza kama hakupatiwa nyaraka juu ya shauri hilo akasema hakupatiwa.

Hata hivyo wakili wa hoteli hizo, Richard Massawe aliyekuwa mahakamani hapo hakutolea ufafanuzi suala hilo endapo kweli mkurugenzi huyo walimshirikisha au la zaidi aliendelea kutoa taarifa mahakamani hapo kuwa shauri lingine lilolokuwa mahakamani hapo la kuwapinga wasimamizi wa mirathi limefika mwisho.

"Mheshimiwa jaji kwa sasa shughuli za uendeshaji kwenye hoteli hizi zitaanza kwa sababu kwa sasa shauri l kuwwpinga wasimamizi wa mirathi na ndugu wamekubaliana hivyo hoteli hizo zitaanza uendeshaji, zitakodishiwa watu wa kuziendesha hivyo wafanyakazi watalipwa na wataendelea na ajira," alisema wakili Massawe.

MABISHANO MAKALI YA KISHERIA

Awali yaliibuka mabushano makali ya kisheria mahakamani hapo baina ya mawakili wa hoteli hizo na Kaimu afisa Kazi mkoni hapa, Emmanuel Mweta juu ya taratibu zilizotumika kufikisha na kuendesha shauri hilo kwenye mahakama kuu kitengo cha kazi.

Wakili Massawe alidai kamishina wa kazi ndiye alipaswa kupeleka na kusimamia shauri hilo kwenye mahakama ya kazi jambo ambalo Kaimu Afisa Kazi mkoa, Mweta alikipinga kwa kile alichosema shauri hilo likikuwa sahihi mahakamani kwani anapifika mahakamani sheria inampa mamlaka ya kamishina wa kazi.


MAWAKILI WA IMPALA NA NAURA SPRING WAMKANA MKURUGENZI MTENDAJI WA HOTELI HIZO. 

Aidha, Wakili Massawe alidai kuwa hoteli hizo hazikupatiwa taarifa juu ya shauri lilikokuwa mahakama kuu masjala ya ardhi  huku akidai hawamtambui, Herode Biliamtwe aliyekuwa akijitambulisha kama afisa mkuu wa hoteli hizo a kwenye mahakama hiyo .

Pia walisema kuwa hawamtambui, Randy Mrema anayedaiwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa hoteli hizo jambo lililomuibua tena mkurugenzi, Pelagia aliyesema kuwa Randy ni mkurugenzi mtendaji ambaye walimteua kwenye kikao cha bodi huku akimuonyesha jaji, Gwao karatasi ambazo hata hivyo hazikupokelewa.

Hata hivyo Kaimu Afisa Kazi mkoa, Mweta alipingana na hoja za Massawe kwa kile alichoieleza mahakama hiyo kuwa Biliamtwe alikuwa akifika mahakamani hapo akiwa ameambatana na mkurugenzi mtendaji wa hoteli hizo, Randy.

Alisema Randy alitambulishwa kwenye ofisi yao kwa nyaraka halali za hoteli hizo zinazoelezea kumteua kushika nafasi hito ambapo walikuwa wakifanya mawasiliano naye kiofisi kipindi chote.

KAIMU AFISA KAZI AWAWEKEA PINGAMIZI 

Kaimu Afisa Kazi mkoa, Mweta aliweka pingamizi shauri hilo lisiendelee kwa kile alichoeleza kuwa mawakili wanaowakilisha hoteli hizo mahakamani hapo hawajawasilisha nyaraka za kuthibitisha wameagizwa hivyo na hoteli hizo.

Akijibu hilo, wakili Massawe alisema kuwa wakili huyo alipaswa kuwasilisha hoja hiyo mapema zaidi huku akidai haina msingi kwani wao wamefuata taratibu sahihi kuwakilisha kampuni hizo mahakamani hapo.

Jaji Gwae ameahirisha shauri hilo mpaka Novemba 30, mwaka huu atakapotolea uamuzi hoja za pingamizi pamoja na maombi ya kuzuia kuuzwa mali za hoteli hizo ingawa alielezea kushangazwa na mawakili wa pande zote kushindwa kuieleza mahakama ni kiasi gani cha frdha kinachodaiwa na wafanyakazi hao.








 

0 Comments:

Post a Comment